Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Mapigano makali yarindima katikati mwa jiji kubwa la Kunduz

Mapigano makali yamekuwa yakiendelea mapema Jumapili kati ya jeshi la Afghanistan na Taliban katikati mwa jiji la mji mkuu wa mkoa wa Kunduz, kaskazini mwa Afghanistan, kulingana na shirika la habari la AFP na maafisa.

Vikosi maalumu vya Afghanisatn vikifanya mafunzo, Julai 17, 2021.
Vikosi maalumu vya Afghanisatn vikifanya mafunzo, Julai 17, 2021. AP - Rahmat Gul
Matangazo ya kibiashara

"Mapigano makali ya mtaa kwa mtaa yanaendelea katika maeneo tofauti ya jiji. Vikosi vya usalama vimeondoka kuelekea uwanja wa ndege," mjumbe wa baraza la mkoa Amruddin Wali ameliambia shirika la habari la AFP.

Jana Jumamosi kundi la Taliban liliuteka mji wa Sheberghan (kaskazini), mji mkuu wa pili wa mkoa chini ya saa 24 baada ya kuteka mji mwingine muhimu wamkoa wa Zaranj (kusini), bila upinzani wowote kutoka vikosi vya Afghanistan.

Miji mikuu mingine ya jimbo iliyo kwenye tishio ni pamoja na Herat magharibi, na miji ya kusini wa Kandahar na Lashkar Gah.

Jeshi la Afghanistan linasema makumi ya wapiganaji wa Kiislamu, pamoja na makamanda wakuu, wameuawa huko Lashkar Gah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.