Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Taliban ladhibiti mji mkuu wa mkoa wa pili, hofu yatanda Kabul

Kundi la Taliban limeuteka mji wa Sheberghan (kaskazini), mji mkuu wa pili wa mkoa chini ya saa 24 baada ya kuteka mji mwingine muhimu.

Kundi la Taliban laendelea kudhibiti baadhi ya maeneo muhimu, Afghanisatan
Kundi la Taliban laendelea kudhibiti baadhi ya maeneo muhimu, Afghanisatan AP - Abdul khaliq
Matangazo ya kibiashara

"Vikosi na maafisa wa [Afghanistan] walikimbilia kwenye uwanja wa ndege," Qader Malia, naibu gavana wa jimbo la Jawzjan, ambalo Sheberghan ni mji mkuu, ameliambia shirika la habri la AFP, wakati wakazi wa mji wa Kabul wameingiliwa na wasiwasi na hofu imezidi kutanda katika mji huo baada ya Taliban kudhibiti mji mkuu mwingine wa mkoa siku moja kabla.

Jimbo la Jawzjan ni ngome ya Marshal Abdul Rashid Dostom, kiongozi hodari wa wanamgambo wa Uzbek.

Ikiwa ngome yake ya Sheberghan ingebaki mikononi mwa Taliban, itakuwa kikwazo kingine kwa serikali, ambayo hivi karibuni iliwataka mabwana wa zamani wa jeshi kujaribu kuzuia maendeleo ya waasi.

Siku ya Ijumaa Taliban ilidhibiti mji mkuu wa mkoa wa Zaranj (kusini), bila upinzani wowote kutoka vikosi vya Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.