Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Taliban wasonga mbele kaskazini, jeshi lajaribu kudhibiti Kunduz

Vikosi vya jeshi la Afghanistan vimezindua mashambulizi huko Kunduz, kaskazini mwa nchi, Jumatatu hii Agosti 9, baada ya Taliban kudhibiti mji huu wa kimkakati, huku raia wakitoroka makaazi yao kufuatia mapigano katika kujaribu kudhibiti mji mkuu, Kabul.

Miji ambayo imetekwa na Taliban.
Miji ambayo imetekwa na Taliban. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati zoezi la kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani, waliopo nchiniAfghanistan kwa karibu miaka ishirini, litakamilika mwishoni mwa mwezi, Taliban imeongeza kasi kwa mashambulizi katika siku za hivi karibuni, wakidhibiti Jumapili miji mikuu mitatu ya mikoa - ikiwa ni pamoja na Kunduz - baada ya kuteka miji mikuu miwili mingine ya mikoa siku ya Ijumaa.

Kulingana na maafisa kadhaa wa jimbo hilo, wataliban wamesonga mbele katika sehemu nyingi za nchi mnamo wiki za hivi karibuni kwa kuteka wilaya moja baada ya nyingine.

Wataliban wanapambana ili kuudhibiti mji mkuu wa jimbo la kaskazini, Kunduz na hapo jana waliweka bendera yao kwenye uwanja mkuu wa jiji hilo. Pamoja na kuteka sehemu kadha,a kundi la Taliban pia linaendesha kampeni ya mauaji kwa kuwalenga maafisa waandamizi wa serikali kwenye mji mkuu, Kabul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.