Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Taliban waua mwandishi mmoja wa habari, na kumteka nyara mwingine

Wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wa Taliban wamemuua mkurugenzi wa kituo cha redio cha Afghanistan huko Kabul na kumteka nyara mwandishi mmoja wa habari katika mkoa wa Helmand, maafisa wa eneo hilo wamesema leo Jumatatu..

Jeshi la Afghanistan linaendelea kupoteza maeneo yake muhimu.
Jeshi la Afghanistan linaendelea kupoteza maeneo yake muhimu. STR AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Watu wenye silaha walimpiga risasi Toofan Omar, mkurugenzi wa kituo cha redio cha Paktia Ghag, ambaye pia alikuwa kiongozi wa shirika moja la haki za binadamu linalotetea vyombo huru vya habari nchini Afghanistan, katika mauaji yaliyokusudiwa katika mji mkuu Jumapili.

"Omar aliuawa na watu wasiojulikana [...) alikuwa mtu maarufu (...) tunalengwa kwa sababu tunafanya kazi kwa kujitegemea," amesema Mujeeb Khelwatgar, mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la 'NAI.

Mamlaka huko Kabul yanashuku wapiganaji wa Taliban kutekeleza shambulio hilo.

Mwezi uliopita, NAI ilisema angalau waandishi wa habari 30 na wafanyakazi katika vyombo vya habari waliuawa, kujeruhiwa au kutekwa nyara na makundi ya wapiganaji mwaka huu nchini Afghanistan.

Katika mkoa wa Helmand kusini, maafisa wamesema wapiganaji wa Taliban walimteka nyara mwandishi wa habari wa eneo hilo, Nematullah Hemat, kutoka nyumbani kwake huko Lashkar Gah, mji mkuu wa mkoa, jana Jumapili.

"Hatujui kabisa ambapo Taliban walimpeleka Hemat (...) Kwa kweli tuko katika hali ya hofu," amesema Razwan Miakhel, mkurugenzi wa kituo cha kibinafsi cha Gharghasht TV, ambapo Hemat alikuwa anafanya kazi.

Msemaji wa Taliban ameliambia shirika la habari la REUTERS kwamba hakuwa na taarifa juu ya mauaji ya Toofan Omar huko Kabul au kutekwa nyara kwa Nematullah Hemat huko Helmand.

Siku ya Ijumaa, Taliban walimuua mkuu wa huduma ya mawasiliano ya serikali ya Afghanistan huko Kabul.

Siku ya Jumapili waliteka miji mikuu mitatu ya mkoa wa Afghanistan: mji kimkakati wa Kunduz, kaskazini mashariki mwa nchi, Sar-e Pul na Taloqan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.