Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Biden: Sijajutia uamuzi wa kuondoa wanajeshi wa Marekani Afghanistan

Rais wa Marekani Joe Biden amewataka viongozi wa Afghanistan kuipigania nchi yao wakati kuu wapiganani wa Taliban wanapoendelea kuchukua maeneo  mbalimbali ya nchi hiyo.

Mapiano kati ya Taliban na vikosi vyajeshi la Afghanistan yamesababisha mamia ya maelfu kuyatoroka makaazi yao huko Kunduz.
Mapiano kati ya Taliban na vikosi vyajeshi la Afghanistan yamesababisha mamia ya maelfu kuyatoroka makaazi yao huko Kunduz. WAKIL KOHSAR AFP
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Pul-e-Khumri, katika mkoa wa Baghlan, Kaskazini mwa nchi hiyo, hivi punde umeanguka mikononi mwa Taliban, ambao sasa wanadhibiti asililia 65 ya nchi nchi hiyo.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema kwamba hajutii uamuzi wake wa kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, akihakikisha kuwa Washington inatimiza ahadi zake zilizotolewa huko Kabul, na kwamba wanajeshi wa Afghanistan walipaswa kuonyesha nia yao ya kupambana na waasi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Jumanne wiki hii, Joe Biden alisema viongozi wa Afghanistan lazima "waungane". "Lazima wapiganie au watetee wenyewe nchi yao," alisema.

Taliban wameongeza mashambulizi yao kote nchini na katika siku za hivi karibuni wamedhibiti miji mikuu kadhaa ya mikoa, baada ya Marekani kuanza kuondoawanajeshi wake .

Waasi hao wa Kiisilamu wameendeleza mashambulizi pembezoni mwa mji mkuu Kabul,kwa lengo la kuuteka mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.