Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Ubalozi wa Marekani Kabul wawataka raia wa Marekani kuondoka Afghanistan

Marekani inawahimiza raia wake kuondoka Afghanistan mara moja wakitumia ndege za kibiashara zilizopo, ubalozi wa Marekani huko Kabul umesema Alhamisi wiki hii katika barua ya onyo kwenye wavuti yake, wakati waasi wa Taliban wanaendelea kusonga mbele katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.

Wanamgambo wa Afghanistan wakiwa kwenye mkutano na vikosi vya ulinzi Juni 23, 2021 huko Kabul.
Wanamgambo wa Afghanistan wakiwa kwenye mkutano na vikosi vya ulinzi Juni 23, 2021 huko Kabul. AP - Rahmat Gul
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuchukua udhibiti wa mji wa kimkakati wa Ghazni, Taliban wamesogea karibu na kilomita 150 na mji mkuu, Kabul, na kupata ushindi mpya baada ya jeshi la Marekani kuondoka nchini humo.

Siku ya Jumatano afisa wa Idara ya Ulinzi ya Marekani, akinukuu habari za ujasusi, aliliambia shirika la habari la REUTERS kwamba waasi wanaweza kuuzingira mji mkuu wa Kabul ndani ya siku 30 na kisha kuchukua udhibiti ndani ya siku 90.

Katika barua hiyo iliyotolewa Alhamisi, ubalozi wa Marekani huko Kabul unaonya kuwa ujumbe wa kidiplomasia hautaweza kusaidia raia wa Marekani.

"Kwa kuzingatia hali ya usalama na kupungua kwa wafanyakazi, uwezo wa ubalozi kusaidia raia wa Marekani nchini Afghanistan ni mdogo sana, hata huko Kabul," kulingana na barua hiyo.

Washington mnamo Aprili 27 iliagiza wafanyikazi wa serikali kuondoka katika ubalozi wa Kabul ikiwa wangeweza kutekeleza majukumu yao wakiwa katika eneo lingine, wakielezea sababu za vurugu zinazoongezeka katika mji mkuu wa Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.