Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Hofu yatanda Kabul wakati Taliban yaendelea kudhibiti miji mikuu ya mikoa

Miji mikuu tisa ya mikoa ilianguka iko mikononi mwa Taliban. Wakaazi wa mji wa Kabul na kote nchini wameingiliwa na hofu na wengi kujiuliza hatima ya taifa lao.

NATO imesema sawa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ina wasiwasi juu ya kiwango kikubwa cha umwagikaji damu, kushambuliwa kwa raia na taarifa juu ya kukiukwa haki za binadamu nchini Afghanistan.
NATO imesema sawa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ina wasiwasi juu ya kiwango kikubwa cha umwagikaji damu, kushambuliwa kwa raia na taarifa juu ya kukiukwa haki za binadamu nchini Afghanistan. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Pul-e-Khumri, katika mkoa wa Baghlan, Kaskazini mwa nchi hiyo, hivi punde umeanguka mikononi mwa Taliban, ambao sasa wanadhibiti asililia 65 ya nchi nchi hiyo.

Kwa upande wake, Umoja wa Ulaya umevalia njuga suala la Afghanistan. Nchi sita wanachama wa Umoja wa Ulaya zimeshauri Brussels kusimamisha zoezi la kuwarudisha nyumbani Waafghanistan kutokana na kuzidi kuzorota kwa usalama nchini humo.

Wakati huo huo Jumuiya ya kijeshi ya NATO imewataka wataliban waache mashambulio na imeilezea hali ya usalama nchini Afghanistan kuwa ni ngumu na ya changamoto kubwa.

NATO imesema sawa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ina wasiwasi juu ya kiwango kikubwa cha umwagikaji damu, kushambuliwa kwa raia na taarifa juu ya kukiukwa haki za binadamu nchini Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.