Mapigano Afghanistan : Kabul na Washington walaumiana kufautia
Vita vya maneneo vyaibuka kati ya Marekani na Afghanistan baada ya Taliban kuyateka maeneo kadhaa ya Afghanistan, huku kila upande ukilaumu wengine, wakati vita vinaendelea.
Imechapishwa:
Marekani inasema inasikitishwa na hatua ya maafisa wa usalama nchini Afghanistan kushindwa kuzuia kundi la Taliban kuendelea kuchukua udhibiti wa miji kadhaa, licha ya kutumia Mabilioni ya Dola kuwapa mafunzo na silaha kwa miaka 20.
Serikali ya Afganistan inailaumlu Marekani kwa kuondoa majeshi yake kama sababu ya kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo, wakati huu ikipanga kuyapa silaha makundi ya wapiganaji kusaidia kupambana na Taliban.
Wapiganaji wa Taliban wamekamata zaidi ya robo ya miji mikuu ya mikoa ya nchi hiyo katika kipindi cha chini ya wiki moja.
Wakati huo huo mjumbe maalum wa Marekani kwa Afghanistan Zalmay Khalilzad yuko Doha ambako anajaribu kuwashinikiza viongozi wa Taliban kukubali mpango wa usitishwaji wa mapigano.