Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Taliban wataka mabadiliko ya amani

Taliban wameagizwa kusalia kwenye milango ya mji mkuu Kabul na wasiingie katika mji huo, mmoja wa wasemaji wa kundi hilo ametangaza Jumapili hii, Agosti 15, wakati waasi wakiuzingira mji mkuu na kuchukuwa udhibiti wa nchi nzima.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afghanistan amesema Jumapili, katika ujumbe wa video, kwamba "mabadiliko ya amani" yako njiani kufanyika haraka kuelekea serikali ya mpito.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afghanistan amesema Jumapili, katika ujumbe wa video, kwamba "mabadiliko ya amani" yako njiani kufanyika haraka kuelekea serikali ya mpito. AFP - WAKIL KOHSAR
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya ndani amesema hakutakuwa na shambulio lolote, lakini kutafanyika zoezi la kukabidhiana madaraka kwa amani kwa serikali ya mpito. Taliban wanaunga mkono utaratibu huo.

Waasi wa Taliban wanarejea madarakani, miaka ishirini baada ya kutimuliwa na muungano wa kijeshi wa kimataifa mnamo mwaka 2001. baada ya shambulizi la Septemba 11 nchini Marekani. Uingiliaji kijeshi wa muungano wa kimataifa ulisababisha wapiganaji wa kundi hilo kusambarati na kutoweka kwa Mullah Omar, mkuu wa Baraza Kuu la Dola la Kiislamu la Afghanistan na mshirika wa Osama Bin Laden.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afghanistan amesema Jumapili, katika ujumbe wa video, kwamba "mabadiliko ya amani" yako njiani kufanyika haraka kuelekea serikali ya mpito. "Waafghanistan hawapaswi kuwa na wasiwasi," amebaini waziri Abdul Sattar Mirzakwal. "Hakutakuwa na mashambulio yoyote katika mji mkuu wa Kabul," ameongeza, wakati rais Ashraf Ghani bado hajazungumza chochote- baada ya hotuba alioitoa katika siku za nyuma.

"Uongozi wa Taliban umeagiza vikosi vyake vyote kusubiri katika milango ya mji wa Kabul, wasijaribu kuingia katika mji huo," amesema Jumapili hii asubuhi, kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid. “Hatutaki raia hata mmoja asiye na hatia kujeruhiwa au kuuawa. Wakazi waliohojiwa na shirika la habari al AFP wameripoti kwamba wamewaona wapiganaji wenye silaha wa Taliban katika kata yao. Lakini "hakuna mapigano", amesema mmoja wao.

Hatima ya rais Ghani matatani

Taliban wamethibitisha kwamba wanataka kuchukuwa tena madaraka nchini Afghanistan bila umwagaji damu, kwa mabadiliko ya amani. Hii inaweza kufanyika kwa siku kadhaa, wameiambia BBC. "Katika siku zijazo, tunataka mabadiliko ya amani" kwa kukabidhiana madaraka, amesema Suhail Shaheen, msemaji wa Taliban aliyeko Qatar, kama sehemu ya kundi linaloshiriki mazungumzo.

Je! Rais yuko kwenye msimamo huo? Ashraf Ghani hatimaye amezungumza Jumapili hii mchana, saa za Ufaransa. Ametoa wito kwa vikosi vya usalama kuhakikisha "usalama wa raia wote unalindwa" kwa kudumisha utulivu wa umma huko Kabul. “Ni jukumu letu na tutafanya kwa njia bora zaidi. Mtu yeyote ambaye anafikiria kuchochea machafuko au uporaji atachukuliwa hatua kali, ”amesema rais Ghani katika ujumbe wa video uliotumwa kwa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.