Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Afghanistan: Biden atuma wanajeshi zaidi kuokoa Wamarekani Kabul

Rais wa Marekani Joe Biden amesema, siku ya Jumamosi aliidhinisha kupeleka vikosi vya ziada vya kijeshi huko Kabul kuwahamisha wafanykazi kutoka ubalozi wa Marekani nchini Afghanistan.

Kabul, Agosti 15: Helikopta ya jeshi la Marekani juu ya Ubalozi wa Marekani. Marekani inawaondoa raia wake.
Kabul, Agosti 15: Helikopta ya jeshi la Marekani juu ya Ubalozi wa Marekani. Marekani inawaondoa raia wake. AP - Rahmat Gul
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, Joe Biden ametetea uamuzi wake wa kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, akisema kuwa vikosi vya Afghanistan vinapaswa kujitetea dhidi ya Taliban.

"Baada ya kusikia mapendekezo ya timu zetu za kidiplomasia, kijeshi na ujasusi, niliidhinisha kutumwa kwa karibu wanajeshi 5,000 wa Marekani kuhakikisha zoezi la kuwaokoa wafanyakazi wetu wa ubalozi," amesema rais wa Marekani.

Joe Biden amesema utawala wake uliwaambia maafisa wa Taliban nchini Qatar kwamba kitendo chochote kitakachohatarisha usalama wa wafanyakazi wa Marekani "kitasababisha majibu ya haraka na ya nguvu ya jeshi la Marekani."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.