Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Umoja wa Mataifa wataka Baraza la Usalama kulinda haki za binadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "kutumia zana zote zinazoweza kuondoa tishio la kigaidi ulimwenguni nchini Afghanistan" na kuhakikisha haki za msingi za binadamu zinaheshimshwa katika nchi hii, baada ya taliban kuchukua kuchukuwa udhibiti wa nchi hiyo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. AP - Maxim Shemetov
Matangazo ya kibiashara

"Tunapokea ripoti za kutisha kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kote nchini. Nina wasiwasi hasa na ripoti za kuongezeka kwa ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya wanawake na wasichana nchini Afghanistan," Antonio Guterres amewaambia wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

"Hatuwezi na hatupaswi kuwatelekeza raia wa Afghanistan," ameaongeza.

Taliban imetangaza ushindi nchini Afghanistan baada ya kuteka mji mkuu Kabul, na kutamatisha karibu miaka 20 ya uwepo wa Marekani na washirika wake nchini humo

Wapiganaji wamechukua ikulu ya rais. Serikali imeanguka, huku Rais Ashraf Ghani akikimbia.

Msemaji wa kundi hilo ameuambia mtandao wa habari wa Al Jazeera: "Vita vimekwisha."

Kabul ulikuwa mji mkuu wa mwisho nchini Afghanistan kudhibitiwa na Taliban, kasi ya udhibiti wa miji ukiwashtua waangalizi wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.