Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Taliban wadhibiti Kabul, nchi za Magharibi zaondoa raia wao

Taliban waliingia Kabul Jumapili, Agosti 15, baada ya jeshi la Afghanistan kufanya kampeni ya kasi, jambo ambalo limewashangaza wengi. Waliteka ikulu ya rais. Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani aliondoka mapema nchini humo. Wanadiplomasia na raia wengine wa kigeni wamekuwa wakihamishwa haraka kutoka mji wa Kabul.

Helikopta ya jeshi la Marekani ikiruka juu ya Ubalozi wa Marekani huko Kabul Agosti 15, 2021.
Helikopta ya jeshi la Marekani ikiruka juu ya Ubalozi wa Marekani huko Kabul Agosti 15, 2021. Wakil KOHSAR AFP
Matangazo ya kibiashara

► Ufaransa: kipaumbele kwa usalama wa raia wa Ufaransa walioko Afghanistan

Rais wa Ufaransa anafuatilia kwa karibu kuzorota kwa hali nchini Afghanistan. Emmanuel Macron anatarajia kuongoza Baraza la Ulinzi leoJumatatu,  na atalihutubia taifa Jumatatu jioni saa mbili usiku (saa za Ufaransa), ikulu ya Elysée imesema.

Ofisi ya rais wa Ufaransa inabaini kwamba kipaumbele cha haraka katika saa zinazokuja ni usalama wa raia wa Ufaransa walioko nchini Afhanistan, na ambao walitolewa wito wa kuondoka nchini humo, na pia wafanyakazi wa Ufaransa na Afghanistan. Lengo pia ni kudumisha uwezo wa kuwalinda raiawa Afghanistan walioshirikiana na jeshi la Ufaransa, na pia waandishi wa habari, wanaharakati wa haki za binadamu, wasanii na viongozi wa Afghanistan walio hatarini.

Wizara ya Mambo ya nje imeamua kuhamishia ubalozi wake katika eneo la uwanja wa ndege wa Kabul.

"Kutokana na kuzorota kwa kasi kwa hali ya usalama nchini Afghanistan, mamlaka ya Ufaransa imeamua kuhamishia ubalozi wake katika eneo la uwanja wa ndege wa Kabul,hali ambayo itawezesha zoezi la kuwaondoa raia wetu wote ambao bado wako nchini Afghanistan" , Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema katika taarifa.

Ubalozi na kituo cha shida na msaada wa Wizara ya Ulaya na Mambo ya nje wanawasiliana na Wafaransa ambao wamejitokeza. Shughuli hizi za uokoaji wa raia wa nchi yetu zimekuwa zikiendelea kwa wiki kadhaa na ndege maalum ilikuwa imekodiwa kuanzia Julai 16 haswa, kufuatia wito kadhaa kutoka kwa wizara kwa raia wetu kuondoka nchini ", inabainisha wizara ya Ufaransa. kutolewa kwa vyombo vya habari.

Ufaransa inatuma kuanzia kesho ndege kubwa ya kijeshi, A400M, kuwahamisha raia wake ambao bado wako Kabul.

► Ujerumani yaanza zoezi la kuondoa wafanyakazi kutoka ubalozi

wakeTangu Jumapili jioni Ujerumani imekuwa ikiwahamisha wafanyikazi wa ubalozi wake huko Kabul, ambao sasa wapo kwenye uwanja wa ndege, ametangaza Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani. "Baadhi yao wataondoka Kabul baadaye leo," Heiko Maas amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Berlin.

Hata hivyo, "ndege za Bundeswehr (jeshi la Ujerumani) zitaondoka Ujerumani jioni hii, kusaidia katika zoezi hilo katika siku zijazo," ameongeza.

► Boris Johnson anatoa wito kwa nchi za Magharibi kuwa na umoja dhidi ya Taliban

Uingereza ilituma wanajeshi 600 nchini Afghanistan kusaidia kuhamisha raia wake. Lakini Balozi Laurie Bristow bado yuko Kabul na ataondoka hapo ikiwa itahitajika.

"Kipaumbele" kwa London, ameelezea Waziri Mkuu Boris Johnson, ni "kutimiza majukumu yake kwa raia wa Uingereza walioko nchini Afghanistan na kwa wale wote ambao wamechangia katika juhudi za Uingereza nchini Afghanistan tangu miaka 20iliyopita".

"Hali bado ni ngumu sana na ni wazi kutakuwa na serikali mpya huko Kabul hivi karibuni," amesema kwenye runinga ya Uingereza. "Kile ambacho Uingereza itafanya ni kushirikiana na washirika wetu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kutoa ujumbe kwamba hatutaki nchi yeyote itambue Taliban. Tunataka msimamo wa pamoja [...]".

Kabul ulikuwa mji mkuu wa mwisho nchini Afghanistan kudhibitiwa na Taliban, kasi ya udhibiti wa miji ukiwashtua waagalizi wengi.

Wanamgambo hao waliweza kuchukua udhibiti baada ya wanajeshi wengi wa kigeni kuondoka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.