Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Angalau watano wafariki dunia katika uwanja wa ndege wa Kabul

Angalau vifo vitano vimeripotiwa katika uwanja wa ndege wa Kabul wakati mamia ya watu wamekuwa wanajaribu kupanda ndege kwa nguvu wakiondoka mji mkuu wa Afghanistan, mashuhuda wameliambia shirika la habari la Reuters.

Afghanistan, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kabul, Agosti 16, 2021, siku moja baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa mji mkuu.
Afghanistan, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kabul, Agosti 16, 2021, siku moja baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa mji mkuu. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Shahidi wa kwanza amesema aliona miili ya watu watano ikisafirishwa kwa gari, lakini wa pili hakuweza kubaini ikiwa waliuawa na risasi au walifariki dunia katika mkanyagano.

Mapema asubuhi ya leo, vikosi vya Marekani vinavyohusika na kuwaokoa raia wa nchi hiyo katika uwanja wa ndege wa Kabul vilipiga risasi hewani kutawanya umati a watu, afisa wa Marekani amesema.

Viongozi hawakupatikana mara moja kutoa maoni juu ya hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.