Pata taarifa kuu
UNSC-AFGHANISTAN

UN: Baraza la Usalama lataka mazungumzo juu ya serikali nchini Afghanistan

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linataka kuundwa, kupitia mazungumzo, serikali mpya nchini Afghanistan ambayo itakuwa ya "umoja, isiyobagua na yenye watu kutoka tabaka mbalmbali ikiwa ni pamoja na wanawake."

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. AP Photo/Mary Altaffer, File
Matangazo ya kibiashara

Wanachama 15 wa Baraza hilo, ambalo lilikutana Jumatatu wiki hii kujadili hali nchini Afghanistan baada ya Taliban kuuteka mji wa  Kabul Jumapili, pia limetaka kukomeshwa mara moja kwa uhasama na ukiukwaji wa haki za binadamu, na ufikiaji wa haraka na bila vikwazo kwa misaada ya kibinadamu kwa walengwa.

Hayo yanajiri wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "kutumia zana zote zinazoweza kuondoa tishio la kigaidi ulimwenguni nchini Afghanistan" na kuhakikisha haki za msingi za binadamu zinaheshimshwa katika nchi hii, baada ya taliban kuchukua kuchukuwa udhibiti wa nchi hiyo.

Taliban imetangaza ushindi nchini Afghanistan baada ya kuteka mji mkuu Kabul, na kutamatisha karibu miaka 20 ya uwepo wa Marekani na washirika wake nchini humo

Wapiganaji wamechukua ikulu ya rais. Serikali imeanguka, huku Rais Ashraf Ghani akikimbia.

Msemaji wa kundi hilo ameuambia mtandao wa habari wa Al Jazeera: "Vita vimekwisha."

Kabul ulikuwa mji mkuu wa mwisho nchini Afghanistan kudhibitiwa na Taliban, kasi ya udhibiti wa miji ukiwashtua waangalizi wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.