Pata taarifa kuu
UJERUMANI-USHIRIKIANO

Ujerumani: Olaf Scholz kuzuru Paris kwa ziara yake ya kwanza ya kiserikali nje ya nchi

Kansela mpya wa Ujerumani Olaf Scholz anawasili Paris Ijumaa hii, ambapo anafanya ziara yake ya kwanza rasmi nje ya nchi. Olaf Scholz atakula chakula cha mchana katika Ikulu ya Elysée pamoja na Rais Macron. Mkutano huo utakuwa fursa kwa viongozi hao wawili kujadili mustakabali wa nchi hizo mbili rafiki na changamoto zinazozingoja katika ngazi ya Ulaya.

Kansela mpya wa Ujerumani Olaf Scholz katika Bunge la Ujerumani tarehe 8 Desemba 2021.
Kansela mpya wa Ujerumani Olaf Scholz katika Bunge la Ujerumani tarehe 8 Desemba 2021. AP - Michael Sohn
Matangazo ya kibiashara

Ushirikiano thabiti wa Ufaransa na Ujerumani ndio Olaf Scholz anataka. Kansela mpya alisema hayo hata kabla ya kuchukua madaraka. Ujerumani ya Olaf Scholz na Ufaransa ya Emmanuel Macron wanataka kuupa Umoja wa Ulaya uhuru zaidi, hasa katika uwanja wa kimataifa.

Makubaliano yanahitajika

Ili kufikia hili, makubaliano kati ya Paris na Berlin ni muhimu. Aidha, wakati Paris inazungumzia uhuru wa kimkakati, Berlin inajibu uhuru wa kimkakati wa Umoja wa Ulaya; washirika hao wawili wanapendelea kufanyia mageuzi mchakato wa kufanya maamuzi mjini Brussels na wangependa kulegeza sheria ya kauli moja kwa nchi ishirini na saba wanachama wa umoja huo.

Lakini pia itahitaji kauli nzuri ya maelewano kati ya Paris na Berlin kwa sababu tofauti ni nyingi. Juu ya jukumu la nguvu za nyuklia katika nishati, kwa mfano, au juu ya ulinzi wa Ulaya; na ni hasa katika mpango wa kuinua uchumi na bajeti ndipo mivutano mikubwa zaidi inatarajiwa.

Marekebisho magumu ya Mkataba wa Utulivu

Waziri mpya wa fedha, Christian Lindner, ni manaharakati mkubwa wa kubana matumizi na utawala wa Ulaya wa upungufu wa juu wa 3%, na mwenzake Bruno Le Maire atakuwa na wakati mgumu kumshawishi kwamba urejeshaji huo unaweka marekebisho ya vigezo vya mkataba wa utulivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.