Pata taarifa kuu

Ujerumani yakumbwa na mlipuko wa nne ambazo wa COVID-19

Kampeni za chanjo dhidi ya Covid zinaendelea lakini sio hakikisho dhidi ya kurudi tena kwa janga hilo. Hii pia ni hali inayoripotiwa nchini Ujerumani ambayo kwa sasa inakabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Mlipuko wa nne wa Covid-19 unasambaa kwa kasi nchini Ujerumani. Hali hiyo inawatia wasiwasi viongozi wakati theluthi mbili ya watu wamepewa chanjo.
Mlipuko wa nne wa Covid-19 unasambaa kwa kasi nchini Ujerumani. Hali hiyo inawatia wasiwasi viongozi wakati theluthi mbili ya watu wamepewa chanjo. Β© THOMAS KIENZLE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu hii, Novemba 8, Ujerumani imeandika rekodi tangu kuzuka kwa janga hili kwa idadi ya zaidi ya kesi 200 kwa kila wakaaji 100,000 kwa siku saba.

Haya yanajiri wakati Baraza la mawaziri la kansela anayeondoka Angela Merkel likiwa njia panda. Mawaziri wanaoondoka hawajaonyesha nia ya kutunga sera nzito kuhusu janga hilo huku mazungumzo yanayoendelea ya kuunda serikali yakiyumba.

Mlipuko wa nne wa Covid-19 unasambaa kwa kasi nchini Ujerumani. Hali hiyo inawatia wasiwasi viongozi wakati theluthi mbili ya watu wamepewa chanjo. Lakini kampeni inakwama kutokana na upinzani kutoka kwa watu wachache wenye upinzani dhidi ya chanjo. Dozi ya tatu ya nyongeza kwa wazee hutolewa kwa kiwango kisichotosha.

Maafisa wa afya wa Ujerumani pamoja na wabunge wanapitia majadiliano magumu kuhusu uwezekano wa wimbi la nne la virusi vya corona na hatua ya kuweka vizuizi vipya vya kupambana na virusi hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.