Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Coronavirus: Ujerumani kupeleka msaada wa matibabu kwa India

Ujerumani itatuma oksijeni na msaada wa matibabu kwa India katika siku zijazo kuisaidia kupambana na kuzuka kwa janga la Corona, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema, wakati marufuku ya wasafiri kutoka India yataanza kutumika leo Jumatatu nchini humo.

Hopitali nyingi nchini India zinakabiliwa na uhaba wa oksijeni, wakati visa vya kila siku vya maambukizi ya virusi vya corona vinaendelea kuongezeka.
Hopitali nyingi nchini India zinakabiliwa na uhaba wa oksijeni, wakati visa vya kila siku vya maambukizi ya virusi vya corona vinaendelea kuongezeka. Manjunath Kiran AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya kila siku ya maambukizi mapya inaendelea kuongezeka nchini India, na rekodi ya visa karibu 350,000 katika kipindi cha saa ishirini na nne iliripotiwa siku ya Jumapili. Hospitali kote nchini zimelazimika kupeleka wagonjwa nyumbani kwa kukosa oksijeni za matibabu.

"India kwa sasa inakumbwa na mlipuko wa pili wenye nguvu isiyo na kifani. Kuchukua hatua haraka ilikuwa chaguo sahihi kuzuia kuingia kwa aina mpya ya kirusi cha Corona nchini Ujerumani," Heiko Maas Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ameliambia Gazeti la Rheinische Post.

Ufaransa na Marekani zajiunga na Ujerumani kwa kusaidia India

Berlin imeiorodhesha India kama nchi yenye hatari kubwa na pia imeiweka kwenye orodha tofauti ya maeneo yenye uangalizi zaidi kwa sababu ya kuibuka kwa aina mpya ya kirusi cha Corona.

Nchi zingine kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ufaransa na Marekani, pia zimetangaza kupeleka msaada wa matibabu kwa India.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.