Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Karibu kesi mpya 12,000 zarekodiwa nchini Ujerumani

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Coronas nchini Ujerumani imepanda hadi 2,414,687, baada ya visa 11,869 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Alhamisi na Taasisi ya magonjwa ya kuambukiza ya Robert Koch (RKI).

Katika kituo cha vipimo kwenye eneo la kiwanda cha nyama wakati wa mlipuko wa Corona, huko Hamm, Ujerumani, Mei 10, 2020.
Katika kituo cha vipimo kwenye eneo la kiwanda cha nyama wakati wa mlipuko wa Corona, huko Hamm, Ujerumani, Mei 10, 2020. REUTERS/Leon Kuegeler
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 385, na kufikisha jumla ya vifo 69,125 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Hayo yanajiri wakati wakuu wa nchi na serikali wa wanachama wa Umoja wa Ulaya unafanyika leo Alhamisi hii, Februari 25 na kuendelea hadi Ijumaa kwa njia ya video.

Hata hivyo ajenda ya mkutano huo ni kuhusu janga la COVID-19. Kuratibu katika mazingira bora vita dhidi ya ugonjwa huo, "kuongeza" kampeni ya chanjo. Lakini suala hilo limewagawanya viongozi hao.

Kwanza, kuhusu suala la mipaka. Pamoja na kuongezeka kwa idadi ya visa inayohusiana na aina mpya ya kirusi cha Corona, nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Ujerumani, Ubelgiji, Denmark, Finland, Sweden na Hungary zimechukua hatua kali za kufunga mipaka yao kulaaniwa vikali mwanzoni mwa wiki na Tume ya Ulaya kwa sababu ya vizuizi vinavyokiuka uhuru wa kutembea katika nchi za Ulaya.

Mkutano unaofunguliwa Alhamisi hii utakuwa ni fursa kwa viongozi hao kushirikiana pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.