Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Uhaba wa chanjo ya COVID-19 kuendelea hadi mwezi Aprili

Uhaba wa sasa wa chanjo dhidi ya virusi vya Corona unatarajiwa kuendelea hadi mwezi Aprili, waziri wa afya wa Ujerumani ameonya leo Alhamisi, wakati serikali ikikabiliwa na ukosoaji zaidi juu ya kampeni yake ya chanjo.

Mgonjwa wa Corona
Mgonjwa wa Corona REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Bado tutakuwa na kipindi kigumu cha angalau wiki kumi tukikabiliwa na uhaba wa chanjo," Jens Spahn amesema katika ujumbe wa Twitter, na kuongeza kwamba alitaka kuitisha mkutano wa viongozi wa shirikisho na mkoa kujadili kuhusu chanjo.

Hayo yanajiri wakati kampeni ya chanjo ya Ulaya inalegelega baada ya kampuni ya AstraZeneca kuonya kuwa haitaweza kufikia malengo yaliyoahidiwa juu ya usafirishaji wa chanjo hiyo kwa mataifa ya Umoja Ulaya wiki moja tu baada ya kampuni ya Pfizer kusema pia inachelewesha kiwango cha usambazi wa chanjo ya COVID-19.

Kisa cha kwanza Ujerumani kiliripotiwa tarehe 27.01 mwaka 2020 ambapo mfanyakazi wa kampuni iliyoko Munich alipatikana na Corona, na kifo cha kwanza cha COVID-19 kiliripotiwa mnamo Machi 8. Siku mbili baadaye, kulikuwa na maambukizi katika majimbo yote 16. Tangu wakati huo, hakuna chochote kilichobaki sawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.