Pata taarifa kuu
UJERUMANI-COVID 19-AFYA

Maambukizi ya Corona yafikia milioni 2 Ujerumani

Ujerumani imerekodi visa zaidi ya milioni mbili vya maambukizi ya COVID-19 tangu kuzuka kwa janga hilo, kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Robert Koch (RKI) kimetangaza leo Ijumaa.

Kirusi cha Corona
Kirusi cha Corona NIAID-RML via AP
Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo yenye watu wengi katika Umoja wa Ulaya imerekodi visa vipya 22,368 vya maambukizi kwa muda wa saa 24 zilizopita, kwa jumla ya visa 2,000,958.

Ujerumani pia umerekodi vifo vipya 1,113 katika kipindi cha siku moja iliyopita, na kufanya jumla ya vifo kufikia 44,994.

Licha ya serikali kuongeza hatua za kukabiliana na maambukizi hali inaendelea kuwa mbaya nchini Ujerumani.

Kansela Angela Merkel na viongozi wa serikli yake wameonya kuwa hatua za kukabiliana na maambukizi zinaweza kuendelea hata baada ya mwezi januari.

Merkel anatarajiwa kukutana na mawaziri wakuu wa majimbo yote 16 ya Ujerumani, baadae mwezi huu kwa ajili ya kujadili hatua zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.