Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 8,000 zarekodiwa nchini Ujerumani

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 2,402,818, baada ya kesi 8,007 kuthibitishwa siku iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Jumatano na Taasisi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ya Robert Koch (RKI).

Watu waliowekwa karantini majumbani mwao baada ya janga la Corona wakipewa chakula, Juni 23, 2020 huko Verl, magharibi mwa Ujerumani.
Watu waliowekwa karantini majumbani mwao baada ya janga la Corona wakipewa chakula, Juni 23, 2020 huko Verl, magharibi mwa Ujerumani. Ina FASSBENDER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 422, na kufikisha jumla ya vifo 68,740 tangu kuzukaa kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Mwezi Desemba 2020 Ujerumani ilianza zoezi la kuiweka nchi nzima katika hali ya kufunga shughuli nyingi za kila siku hadi tarehe 10 mwezi Januari 2021 kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Ujerumani kama nchi nyingine barani Ulaya inaendelea kjukabiliana na janga hili hatari, ambalo limesababisha vifo vingi katika bara hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.