Pata taarifa kuu

Watu ambao hawajapata chanjo kukabiliwa na vizingiti Ujerumani

Kirusi kipya cha Covid-19, Omicron, kinaendelea kuzua wasiwasi duniani, wakati huu mataifa mbalibali barani Ulaya na Marekani yakichukua hatua za kudhibiti kusambaa kwa kirusi hicho.

Bango linaloonyesha sheria inayoitwa 2G (wale tu waliochanjwa au kupona Covid-19), kwa soko la Krismasi katika jiji la Dortmund, magharibi mwa Ujerumani, Desemba 1, 2021.
Bango linaloonyesha sheria inayoitwa 2G (wale tu waliochanjwa au kupona Covid-19), kwa soko la Krismasi katika jiji la Dortmund, magharibi mwa Ujerumani, Desemba 1, 2021. AFP - INA FASSBENDER
Matangazo ya kibiashara

Nchini Ujerumani, serikali imepiga marufuku watu ambao hawajachanjwa kutoruhisiwa kuingia katika maeneo ya umma kama, mikahawani, majumba ya kumbi za sinema, maduka makubwa na maeneo mengine yenye mikusanyiko mikubwa ya watu.

Kansela Angela Merkel anayemaliza muda wake, amesema hatua zimekuja ili kuzuia kusambaa kwa kirusi hicho, lakini pia serikali inatafakari, kuhakikisha kuwa utoaji wa chanjo unakuwa kwa lazima kufikia mwezi Februari.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema kumbi za maonyesho ya sanaa na kumbi za sinema zitafunguliwa kwa ajili ya watu waliopata chanjo na kuongeza kuwa hatua kama hiyo itahusisha maduka ya bidhaa zisizo za lazima. 

Nchini Marekani, kirusi kipya cha Omicron sasa kimefika katika majimbo matano ya California, Colorado, Minnesota, New York na  Hawaii, na inaelezwa kuwa walioambukizwa hawana historia ya kusafiri.

Serikali ya rais Joe Biden sasa imetoa masharti mapya, abiria wote wanaowasili nchini humo, watatakiwa kupimwa virusi hivyo saa 24 kabla ya safari na uvaaji wa barakoa utaendelea mpaka mwezi Machi.

Mataifa 30 duniani hasa barani Ulaya yanaripoitiwa kukumbwa na kirusi hiki kipya ambacho kinazua wasiwasi kote duniani, huku watalaam wakihpfia kuwa huenda kirusi hiki kikasambaa kwa kasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.