Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Tafiti : Emmanuel Macron kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais Ufaransa

Nchini Ufaransa, tafiti zimeonesha kwamba raia nchini humo wana uhakika kwamba Rais wa sasa Emmanuel Macron ana nafasi kubwa ya kuibuka mshindi katika mzunguko wa kwanza wakati uchaguzi huo utakapofanyika Aprili 10.

Mabango ya wagombea urais katika mitaa ya Ufaransa.
Mabango ya wagombea urais katika mitaa ya Ufaransa. AFP - SEBASTIEN SALOM-GOMIS
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kura ya maoni ya kampuni ya BVA iliyotolewa Ijumaa wiki iliyopita, asilimia 75 ya raia waliosajiliwa nchini humo, wana nia ya kupiga kura, japo wakati huu asilimia hiyo itashuka ikilinganishwa na mwaka 2017. 

Mgombea Urais Marine Le Pen ameonekana kama atakayefika kwenye duru ya pili ya Uchaguzi na Macron, ambapo watakutaka kwenye duru hiyo jinsi walivyofanya mwaka 2017, japo pia mgombea  Jean-Luc Melenchon ameongeza umaarufu wake katika siku za hivi maajuzi. 

Kura ya maoni ya hivi punde iliyochapishwa na Ifop-Fiducial siku ya Jumatatu, imeonyesha Macron akiongoza kwa asilimia 28 huku Le Pen akimfuata nyuma na asilimia 21 katika duru ya kwanza ya uchaguzi. 

Tahariri katika gazeti la kila siku la Ufaransa la Le Monde, ilitoa mfano wa kura ya maoni ya Ipsos-Sopra Steria iliyoidhinisha kwamba ilitabiri kujitokeza kwa asilimia 67 katika awamu ya kwanza, siku ya Jumatatu ikionya kuhusu hatari iliyopo, wakati huu kuna ongezeko la mfumuko wa bei, mabadiliko ya hali ya hewa, na vita vinavyoendelea nchini Ukraine. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.