Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Joto la kisiasa lapanda kuelekea uchaguzi wa urais Ufaransa

Nchini Ufaransa, kampeni za kisiasa zimeshika kasi, kuelekea Uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Aprili 10, wakati huu kura za maoni zikionesha kuwa, rais Emmanuel Macron ana nafasi kubwa ya kushinda.

Iwapo hakutakuwa na mshindi atakayepata asililia 50 ya kura katika mzunguko wa kwanza Aprili 10, wagombea wakuu wawili watamenyana katika mzunguko wa pili Aprili tarehe 24.
Iwapo hakutakuwa na mshindi atakayepata asililia 50 ya kura katika mzunguko wa kwanza Aprili 10, wagombea wakuu wawili watamenyana katika mzunguko wa pili Aprili tarehe 24. REUTERS - STEPHANE MAHE
Matangazo ya kibiashara

Mbali na rais Macron, kuna wagombea wengine 11 wanaotafuta uongozi wa taifa hilo la barra Ulaya.

Wadadisi wa siasa za Ufaransa wanasema umaarufu wa Macron umeongezeka kwa kiasi kubwa katika siku za hivi karibuni kutokana na juhudi zake wa kidiplomasia kwa namna alivyoshughulikia vita nchini Ukraine na siku Jumatatu amekutana na wanafunzi kutafuta uungwaji mkono.

Marine Le Pen mwanasiasa mkongwe anayeegemea siasa za mrengo wa kushoto ambaye umaarufu wake umeonekana kuongzeka mwezi Machi, alizomewa na wapiga kura katika kisiwa cha Guadeloupe, wakimwita mbaguzi.

Le Pen sera yake imekuwa ni  kurejesha tamaduni za Ufaransa, na kufanya Ufaransa kuwa ya Wafaransa kwanza,  mtazamo ambao pia unaendana na ule wa mgombea mwingine Eric Zemmour, ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano wake jijini Paris, huku wafuasi wake wakitamka “Macron assassin”au muueni Macron, katika mkutano anaosema uluhudhuriwa na watu zaidi ya Laki Moja.

Aidha, wagombea wengine wanaotajwa kutoa ushindani na kusababisha uchaguzi huo kufika katika mzunguko wa pili ni pamoja na Valerie na mwanasiasa wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Melenchon.

Iwapo hakutakuwa na mshindi atakayepata asililia 50 ya kura katika mzunguko wa kwanza Aprili 10, wagombea wakuu wawili watamenyana katika mzunguko wa pili Aprili tarehe 24.

Baada ya kuanza kwa kampeni, vyombo vya Habari nchini humo vinatakiwa kutoa muda sawa kwa wagombea wote wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.