Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Ripoti: Macron apewa nafasi kubwa ya kutetea wadhifa wake katika uchaguzi wa urais

Nchini Ufaransa, kura mpya ya maoni inaonesha kuwa, rais Emmanuel Macron ameendelea kupata uungwaji mkono wa wapiga kura, kuelekea Uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi Aprili. 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. REUTERS - PIROSCHKA VAN DE WOUW
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii imekuja, baada ya Macron siku ya Alhamisi kuthibitisha kuwa atawania tena uongozi wa nchi hiyo, kuongoza kwa muhula wa pili. 

Uchunguzi uliofanywa na shirika la BVA, umebaini kuwa Macron ameimarisha umaarufu wake kwa namna alivyoongoza uongozi kushughulikia mzozo wa Urusi na Ukraine. 

Imebainika kuwa, iwapo uchaguzi ungefanyika leo, kiongozi huyo wa Ufaansa angemaliza wa kwanza kwa kupata asilimia 29 ya kura katika mzunguko wa kwanza na kupata ushindi katika mzunguko wa pili, licha ya upinzani kutoka kwa Marine Le Pen anayetajwa kuwa mshindani wa karibu. 

Kupitia barua kwa wapiga kura, Macron mwenye umri wa miaka 44, amesema anawaomba imani yao kwa miaka mitano ili kutetea miiko iliyo kwenye hatari ya kutoweka.

Wanasiasa wengine wanaotarajiwa kupambana na Macron ni pamoja na Anne Hidalgo kutoka chama cha Kisosholisti, Jean-Luc Melenchon na Eric Zemmour anaegemea siasa za mrengo wa kulia. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.