Pata taarifa kuu

Vita Ukraine: Macron ataka kujifunza somo la uvamizi wa Urusi katika ngazi ya Ulaya

Wakati wa hotuba yake ya televisheni kuhusu vita vya Ukraine, rais wa Ufaransa ametangaza kufanyika kwa mkutano usio rasmi wa kilele wa Ulaya mnamo Machi 10 na 11 huko Versailles ambao "itabidi kuamua" juu ya "mtindo mpya wa kiuchumi" wa Umoja wa Ulaya, EU, kutokana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake ya televisheni, Machi 2, 2022.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake ya televisheni, Machi 2, 2022. © AFP/Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

"Kurejea kwa hali hii ya kikatili katika Historia, lazima tujibu kwa maamuzi ya kihistoria," amesema Emmanuel Macron katika hotuba ya televisheni muda mfupi baada ya kushutumu uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine kama vita "iliyochochewa na usomaji wa marekebisho ya historia ya Ulaya" . “Ulaya yetu tayari imeonyesha umoja na dhamira. Imeingia katika enzi mpya,” ameongeza.

Mkutano usio rasmi wa kilele wa Umoja wa Ulaya, ulioandaliwa katika huko Versailles, karibu na Paris, kama sehemu ya uenyekiti wa Ulaya kwa zamu ya Ufaransa, kwa hivyo itabidi kuchukua maamuzi juu ya "mkakati wa uhuru wa nishati ya Ulaya" na "ulinzi wa Ulaya". Hapo awali, mkutano huu ulikuwa wa kuzingatia "mfano wa ukuaji wa uchumi na uwekezaji wa Ulaya kwa mwaka 2030", kufuatia mpango mkubwa wa uokoaji ulioanzishwa na umoja huo katikati ya mgogoro wa kiafya uliosababishwa na Covid-19.

Ulaya "lazima sasa ikubali kutetea amani"

Ulaya “lazima sasa ikubali kutetea amani, uhuru na demokrasia. Ni lazima kuwekeza zaidi kutegemea kidogo mabara mengine na kuweza kujiamulia yenyewe, kwa maneno mengine kuwa mamlaka huru zaidi, yenye mamlaka zaidi,” ametangaza Emmanuel Macron.

“Nguvu ya amani, hatuwezi kutegemea wengine watutetee, iwe juu ya nchi kavu, baharini, chini ya bahari, angani, […] Ulinzi wetu wa Ulaya lazima uchukue hatua nyingine,” ameongeza.

"Hatuwezi tena kutegemea wengine, na hasa gesi ya Urusi, kututembeza, kutupa joto, kuendesha viwanda vyetu. Hii ndiyo sababu, baada ya kuamua, kwa Ufaransa, maendeleo ya nishati mbadala na ujenzi wa vinu vipya vya nyuklia, nitatetea mkakati wa uhuru wa nishati ya Ulaya ", amebaini rais wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.