Pata taarifa kuu

Ukraine: Baada ya mazungumzo na Putin, Macron afikiria kuwa 'mashambulizi zaidi yanakuja'

Wanajeshi wa Urusi wameingia leo katikati ya mji wa bandari wa Kherson nchini Ukraine, siku moja baada ya madai yanayokinzana kuhusu kama Moscow imeukamata mji wowote mkubwa nchini humo kwa mara ya kwanza katika uvamizi wake wa siku nane. 

Kyiv, Machi 3, 2022.
Kyiv, Machi 3, 2022. AP - Efrem Lukatsky
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo mapya yamepangwa kufanyika Alhamisi huku makombora ya Urusi yakiendelea katika miji kadhaa. Mji wa Mariupol unakaribia kutengwa na ulimwengu na unaendelea kukumbwa mashambulizi mengi ya mabomu.

Wakati huo huo Urusi imeongeza mashambulizi yake kwenye miji ya bandari, lakini pia katika maeneo ya magharibi zaidi, karibu na mpaka wa Poland. Jiji la Mariupol linapitia wakati mgumu, kulingana na meya wa mji huo. Pia yanalengwa na mashambulizi mengi ya mabomu, kama vile Kharkiv na Kiev zilivyokuwa jana usiku.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelihutubia taifa, huku. akisema kumuunga mkono mwenzake wa Ukraine na akashutumu vita "iliyochochewa na usomaji wa marekebisho ya historia ya Ulaya".

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa wingi azimio la kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Wakimbizi milioni moja tayari wamekimbia mapigano, kulingana na ripoti mpya kutoka Umoja wa Mataifa. Katika mipaka ya Ukraine, kuna maelfu wanaosubiri kuvuka na kwenda nchi jirani.

Mazungumzo mapya kati ya Ukraine na Urusi yamepangwa kufanyika Alhamisi, Machi 3

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.