Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Urais: Emmanuel Macron arasimisha kuwania kwake katika barua kwa Wafaransa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alirasimisha nia yake ya kugombea kwa muhula wa pili Alhamisi Machi 3 katika "Barua kwa Wafaransa" iliyochapishwa kwenye tovuti za magazeti ya kila siku ya kikanda.

Kwa kurasimisha ugombea wake urais baada ya miezi kadhaa ya mashaka ya uwongo, Emmanuel Macron anaanza moja ya kampeni fupi zaidi kufanywa na rais anayemaliza muda wake.
Kwa kurasimisha ugombea wake urais baada ya miezi kadhaa ya mashaka ya uwongo, Emmanuel Macron anaanza moja ya kampeni fupi zaidi kufanywa na rais anayemaliza muda wake. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Alisubiri hadi dakika ya mwisho. Akijihusisha na mgogoro wa kiafya na kisha na vita nchini Ukraine, Emmanuel Macron hatimaye alirasimisha kuwaia kwake kwa uchaguzi wa urais mwezi Aprili maka huu katika barua iliyowekwa mtandaoni Alhamisi hii. Na wakati huu wagombea kwenye kiti cha urais wana hadi Ijumaa saa 6 mchana kurasimisha kuwaia kwao mbele ya Mhakama ya Katiba. Huku zikiwa zimesalia siku 38 kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi, rais wa jamhuri anaweza kuanza kampeni ya uchaguzi iliyovurugwa kwa kiasi kikubwa, mojawapo ya kampeni fupi zaidi kuwahi kufanywa na rais anayeondoka madarakani.

"Mimi ni mgombea wa kubuni nanyi, katika kukabiliana na changamoto za karne hii, majibu ya kipekee ya Ufaransa na Ulaya. Mimi ni mgombea wa kutetea maadili yetu ambayo machafuko ya ulimwengu yanatishia. Mimi ni mgombea ili kuendelea kuandaa mustakabali wa watoto wetu na wajukuu zetu. Kuturuhusu leo ​​na kesho kujiamulia wenyewe,” aliandika.

Katika maandishi haya ya kurasa tatu, rais anayemaliza muda wake anatoa maoni kadhaa juu ya nafasi kuu na maadili yanayohusiana na mradi wake. "Tutalazimika kufanya kazi zaidi na kuendelea kupunguza ushuru wa wafanyikazi na uzalishaji", alitangaza, akiahidi kupambana dhidi ya ukosefu wa usawa. Vito vya kuwahuumia wazee hivi majuzi vimekuwa mada ya mzozo mkali.

Tangazo hili halikuwa jambo la kushangaza. Emmanuel Macron mwenyewe amegusia hilo mara kadhaa na timu yake nzima ya kampeni haikuficha kuwa kila kitu kilikuwa tayari.

Wanaoongoza katika kura za maoni

Emmanuel Macron amejitangaza mwenyewe baada ya wagombea wawili waliomtangulia kwa muhula wa pili. Jacques Chirac mwaka 2002 na Nicolas Sarkozy mwaka 2012 walitangaza kuwania katika kiti cha urais miezi miwili kabla ya uchaguzi. François Mitterrand pekee mwaka wa 1988 na Charles de Gaulle mwaka wa 1965 ndio waliosubiro hata zaidi, karibu mwezi mmoja kabla ya duru ya kwanza. Kusubiri huko kulikashifiwa vikali na wapinzani wa rais anayemaliza muda wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.