Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Ufaransa: Wanasiasa waendelea kunadi sera zao kuelekea uchaguzi wa urais Jumapili

Nchini Ufaransa, kuelekea siku ya mwisho ya kufanya kampeni hapo kesho, leo wagombea wa urais wamepanga mikutano mbalimbali kuendelea kuomba kura

Picha inayoonesha wagombea kumi na wawili wa uchaguzi wa rais wa Ufaransa.
Picha inayoonesha wagombea kumi na wawili wa uchaguzi wa rais wa Ufaransa. REUTERS - STAFF
Matangazo ya kibiashara

Siku moja kabla ya kumalizika kwa kampeni nchini humo, kuelekea uchaguzi siku ya Jumapili, wananchi wa Ufaransa watakapopiga kura kumchagua rais, kura za maoni zinaendelea kuonesha kuwa kinyang’anyiro ni kati ya rais Emmanue Macron na Marine Le Pen. 

 

Wagombea 12 wanatafuta nafasi ya kuingia Ikulu ya Elysée na sasa hatima yao ipo mikononi mwa wapiga kura, hasa kuwavutia wale ambao hawajafanya maamuzi. 

Uchaguzi wa Jumapili utafanyika katika kipindi ambacho Ufaransa kama mataifa mengine duniani, inapopata madhara ya vita vya Ukraine na Urusi, ambavyo vimesabisha kupanda kwa gharama ya maisha pamoja na bei ya mafuta. 

Jana rais Macron na Le Pen walipata nafasi ya kuelezea sera zao kupitia Televisheni ya TF1. Macton akiahidi kushughulia suala ya kustafau kwa watumishi wa umma huku Le Pen akiahidi kupunguza utozwaji wa kodi kwenye umeme kutoka asililia 18 hadi 5 na kuondoa kodi kwenye bidhaa muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.