Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Uchaguzi Ufaransa 2022 : Kiwango cha ushiriki katika uchaguzi chafikia 25.48%

Wapiga kura milioni 48.7  nchini Ufaransa wanapiga kura Jumapili hii Aprili 10, 2022, katika duru ya kwanza kumchagua rais wao mpya, wakati huu wadadisi wa siasa nchini humo wakitabari kuwa, kutakuwa na ushindani kati ya rais Emmanuel Macron na mwanasiasa wa siasa za mrengo wa kulia Marine Le Pen.

Wapiga kura wakipiga kura huko Le Touquet Aprili 10, 2022.
Wapiga kura wakipiga kura huko Le Touquet Aprili 10, 2022. AP - Thibault Camus
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa, kiwango cha wapiga kura walioshiriki katika zoezi la upigaji kura tangu asubuhi hadi saa sita mchana kimefikia asilimia 25.48.

Kiwango cha watu walioshiriki kupiga kura tangu asubuhi hadi saa sita mchana kimefikia asilimia 25.48.
Kiwango cha watu walioshiriki kupiga kura tangu asubuhi hadi saa sita mchana kimefikia asilimia 25.48. © Ministère de l'Intérieur

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa tangu saa mbili asubuhi saa za Paris, lakini raia wa Ufaransa wanaoishi nje ya nchi na wale wanaoshi katika visiwa vinavyomilikiwa na nchi hiyo, walipiga kura jana Jumamosi.

Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kufahamika leo Jumapili usiku, huku wadadisi wa siasa wakisema Macron atatofautiana na mpinzani wake Le Pen kwa asilimia kidogo na hivyo wawili hao watachuana katika duru ya pili Aprili 24.

Ili kumpata mshindi katika duru ya kwanza, mgombea anapaswa kupata asilimia 50 ya kura zote.

Mbali na Macron na Le Pen, kuna wagombea wengine 10 wanaosaka nafasi ya kuongoza taifa hilo la Ulaya, akiwemo mwanasiasa mkongwe mwenye siasa za mrengo wa kushoto Jean-Luc Melenchon, ambaye huenda akamaliza katika nafasi ya tatu.

Kuna wasiwasi kuwa, huenda robo ya wapiga kura, wasijokeze kupiga kura hii leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.