Pata taarifa kuu

Wagombea urais wahutubia wafuasi wao baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi

Wagombea wawili pekee kati ya wagombea kumi na wawili waliosiriki kinyang’anyiro hiki cha uchaguzi wa urais ndio ambao wamefuzu kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi baada ya kupata kura zinazohitajika kuingia katika mzunguko huo.

Emmanuel Macron na Marine Le Pen ndio wagombea wawili walifuzu katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais.
Emmanuel Macron na Marine Le Pen ndio wagombea wawili walifuzu katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Rais anayemaliza muda wake Emmanuel Mcron wa chama cha La République en Marche amepata 28.1%, naye , Marine Le Pen chama cha Rassemblement National almepata 23.3%. Wawili awa watachuana katika duru ya pili itakayofanyika Aprili 24.

Marine Le Pen, anajianda kupepetana na Emmanuel Mcron katika duru ya pili ya uchaguzi.
Marine Le Pen, anajianda kupepetana na Emmanuel Mcron katika duru ya pili ya uchaguzi. AFP - THOMAS SAMSON

Katika hotuba zao mbele ya wafuasi wao baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi, wagombea mbalimbali walipongea jinsi uchaguzi huo ulifanyika katika mazingira ya kuridhisha.

Jean-Luc Mélenchon, mgombea aliyepeperusha bendera ya chama cha La France Insoumise amesema "ukurasa mpya wa mapambano unafunguliwa". Jean-Luc Mélenchon ambaye amewataka wafuasi wake kupunguza hasira amesema "tunajua ambaye hatutampigia kura kamwe.

Amewataka wafuasi wake kutompigia kura Marine Le Pen.

Jean-Luc Mélenchon, mgombea urais wa chama cha La France Insoumise, wakati wa hotuba yake baada ya kutangazwa kwa matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais.
Jean-Luc Mélenchon, mgombea urais wa chama cha La France Insoumise, wakati wa hotuba yake baada ya kutangazwa kwa matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais. © REUTERS/Sarah Meyssonnier

Kwa upande wake Marine Le Pen amewataka wafausi wake na raia wengine kutompigia kura rais anayemaliza muda wake Emmanuel Macron.

"Wale wote ambao hawajaMpigIa kura Macron wanaombwa kujiunga na chama chetu", amesema Marine alipohutubia wafuasi wake.

 

Eric Zemmour: “Asante sana kwa imani na matumaini yeko. Ninaweza kutoa ahadi: Nitaendelea kutetea Ufaransa na mawazo yetu na nina hakika kwamba hivi karibuni tutashinda. Ujumbe wangu umesikika. Nilifanya makosa, ninakiri.”

Amewataka wafuasi wake kumpigia kura Marine Le Pen.

Éric Zemmour akizungumza na wafuasi wake baada ya kushindwa kufikia duru ya pili ya uchaguzi wa urais.
Éric Zemmour akizungumza na wafuasi wake baada ya kushindwa kufikia duru ya pili ya uchaguzi wa urais. © REUTERS/Yves Herman
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.