Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Nicolas Sarkozy kumpigia kura Emmanuel Macron

Aliyekuwa rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, ametangaza kuwa atampigia kura, rais Emmanuel Macron, katika mzunguko wa pili wa uchaguzi wa urais, Aprili 24 dhidi ya mpinzani wake Marine Le Pen. 

Sarkozy aliyeongoza Ufaransa kati ya mwaka 2007 mpaka 2012.
Sarkozy aliyeongoza Ufaransa kati ya mwaka 2007 mpaka 2012. © AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Sarkozy aliyeongoza Ufaransa kati ya mwaka 2007 mpaka 2012 kupitia ukurasa wake wa facebook, amesema atampigia kura Macron kwa sababu, ana uzoefu unaohitajika wakati huu kukiwa na mgogoro wa kimataifa, sera yake ya kiuchumi na ameendelea kuonesha uongozi barani Ulaya. 

Hatua hii imekaribishwa na washirika wa Macron ambao wamesema kiongozi huyo anayesaka tiketi ya muhula wa pili, yuko tayari kwa ajili ya mazungmzo kuhusu mpango wake wa mageuzi katika hifadhi ya jamii kwa wanaostaafu. 

Hata hivyo, Le Pen anasema hatua hii haina dhamira ya kweli na badala yake ni ya kutafuta kura kuelekea uchaguzi wa marudio. 

Akifanya kampeni Kaskazini mwa Ufaransa, Macron amesema yuko tayari kuongeza umri wa watu kuustafu kutoka miaka 62 hadi 64 na sio 65 kama ambavyo amekuwa akipanga ili kufanikiwa kuwalipa waastafu wote, suala ambalo linaonekana kutounga mkono na Wafaransa wengi. 

Kwa upande wake, Le Pen yeye anaahidi kuacha umri wa kuustafu kuwa 62 na kwa wale waliofanya kazi wakiwa na umri wa miaka 20, umri wao wa kuustafu utakuwa 60. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.