Pata taarifa kuu

Kampeni zaendelea kuelekea duru ya pili ya uchaguzi Ufaransa

Nchini Ufaransa, kampeni zinaendelea kushika kasi kati ya wagombe wakuu wawili, rais Emmanuel Macron na Marine Le Pen kuelekea mzunguko wa pili wa uchaguzu wa urais Aprili 24.

Kama ilivyokuwa 2017, Emmanuel Macron na Marine Le Pen watachuana katika duru ya pili ya uchaguzi wa Urais mnamo Aprili 24.
Kama ilivyokuwa 2017, Emmanuel Macron na Marine Le Pen watachuana katika duru ya pili ya uchaguzi wa Urais mnamo Aprili 24. AP - Bob Edme
Matangazo ya kibiashara

Leo, Le Pen mgombea wa siasa za mrengo wa kulia, amekuwa akielezea sera yake ya kigeni, ameahidi iwapo atashinda serikali yake itakuwa na ushirikiano wa karibu kati ya Urusi na NATO, lakini Ufaransa itajiondoa kwenye komandi ya jeshi hilo.

Naye rais Macron  akiwa Mashariki mwa Ufaransa, ametetea mpango wake wa kuhakikisha kuwa Umoja wa Ulaya unakuwa imara.

 Wakati hayo yakijiri, Macron amekanusha uvumi kuwa ameingia kwenye mkataba na rais wa zamani Nicholas Sarkozy ambaye ametangaza atamuunga mkono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.