Pata taarifa kuu

WHO yakosoa nchi kadhaa za Ulaya kwa 'kuondoa' hatua za kukabiliana na Covid-19

Nchi kadhaa za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ujerumani, Ufaransa, Italia na Uingereza, zimeondoa hatua zao za kukabiliana dhidi ya Covid pia "kikatili" na kujikuta zinakabiliwa na ongezeko kubwa la kesi aina ya BA.2, Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema leo Jumanne.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani barani Ulaya, Hans Kluge.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani barani Ulaya, Hans Kluge. © AP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Moldova, mkurugenzi wa WHO barani Ulaya, Hans Kluge, amesema yuko "macho" juu ya hali ya sasa ya janga katika bara hilo, huku akidai kuwa bado ana "matumaini".

Kwa sasa, idadi ya kesi za Covid inaongezeka katika nchi 18 kati ya 53 katika bara , kulingana na shirika hilo la kimataifa afya.

"Nchi ambazo tunaona baadhi ongezeko fulani ni Uingereza, Ireland, Ugiriki, Cyprus, Ufaransa, Italia na Ujerumani," Kluge amesema.

"Nchi hizi zimeondoa ghafla vikwazo kutoka kwa kiwango cha + kupita kiasi + hadi + haitoshi +", amebaini afisa huyo wa Umoja wa Mataifa.

Kulingana na takwimu za WHO, idadi ya kesi mpya barani Ulaya ilikuwa imepungua sana baada ya rekodi ya visa mwishoni mwa mwezi Januari, lakini imekuwa ikiongezeka tangu mapema mwezi Machi.

Kulingana na wataalamu wa magonjwa, kuongezeka kwa visa vya maambukizi kunafafanuliwa hasa na wingi wa aina mpya ya kirusi cha Omicron BA.2, ambayo inaambukia kwa takriban 30% - lakini sio hatari zaidi - kuliko kirusi kilichotangulia cha BA.1.

Katika siku saba zilizopita, zaidi ya visa vipya milioni 5.1 na vifo 12,496 vimerekodiwa katika eneo la WHO Ulaya, na kufanya jumla ya kesi zilizogunduliwa tangu kuanza kwa janga hilo kufikia karibu milioni 194.4 na idadi ya vifo kufikia zaidi ya milioni 1.92.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.