Pata taarifa kuu
AFRIKA-USHIRIKIANO

Daktari Nkengasong asifu viongozi wa Afrika kwa jitihada zao dhidi ya Covid-19

Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa kwenye Umoja wa Afrika Daktari John Nkengasong, amesema viongozi wa mataifa ya Afrika, walichukulia kwa makini maambukizi ya virusi vya Covid-19 tangu kuzuka kwa janga hilo kuanzia mwaka 2020.

John Nkengasong, CDC, John Nkengasong.
John Nkengasong, CDC, John Nkengasong. AFP/Michael Tewelde
Matangazo ya kibiashara

Dokta Nkengasong ameiambia Televisheni ya France 24 kuwa ameshirikiana kwa karibu na viongozi wa mataifa ya Afrika kupambana na janga la Covid-19.

Kwa ujumla ushirikiano katika kubiliana na janga la COVID 19 umekuwa mzuri sana; kwa sababau viongozi wa kisiasa walichukilia ugonjwa huu kwa uzito mkubwa sana, na kwa kushirkiana na Mkuu wa Tule ya Umoja wa Afrika Moussa Faki, tulitoa ripoti  mara 16 kuhusu mwenendo wa  janga hili, huu ni ushirikian wa kipekee kwa viongozi wa nchi kuonesha ushirikiano kama huu.

Hayo yanajiri wakati lengo la kufikia 40% ya viwango vya chanjo kamilifu katika kila nchi hadi kufikia mwisho wa mwezi Disemba halijafanikiwa barani Afrika.

Shirika la Afya Duniani (WHO) liliweka lengo hilo mapema mwaka huu, lakini ni takribani asilimia 9 tu ya watu barani Afrika wamepatiwa chanjo kamili hadi sasa.

Ni nchi saba pekee barani zimefikia lengo la 40%. Tatu kati ya hizi ni mataifa ya visiwa vidogo ambapo changamoto za vifaa ni rahisi kukabiliana nazo. Seychelles na Mauritius zimechanja kikamilifu zaidi ya 70% ya wakazi wake, huku Cape Verde ikichanja karibu 45%.

Katika nchi za bara ni Morocco, Tunisia, Botswana na Rwanda pekee ndizo zimevuka lengo hilo.

Nchi za kusini mwa bara zinafanya vizuri zaidi kuliko maeneo mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara

Mpaka kufikia Desemba 30, nchi chini ya nusu katika bara hilo zilikuwa zimepata chanjo kamili kwa zaidi ya 10% ya watu wote (lengo ambalo WHO iliweka kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba, na ambalo halijafikiwa na mataifa mengi ya Afrika).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.