Pata taarifa kuu

Wabunge kadhaa Kenya wakutwa na kirusi cha Omicron baada ya kupimwa

Idadi kubwa ya wabunge na wafanyakazi katika bunge la Kenya wamepatikana na kirusi kipya cha Omicron na wametakiwa kujitenga kwa mujibu wa mwongozo wa wizara ya afya, amesema Karani wa Bunge la Taifa, Michael Sialai, huku amekiri kuwa afisi yake inafahamu kuwa kuna usambaaji wa virusi hivyo baada ya wafanyakazi kupimwa.

Makao makuu ya Bunge la Kenya, jijini Nairobi.
Makao makuu ya Bunge la Kenya, jijini Nairobi. Kevin MIDIGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makumi ya wabunge na wafanyakazi wa idara ya bunge nchini Kenya wameambukizwa Covid-19, baada ya kurejea kutoka nchi jirani ya Tanzania walipokuwa kwenye michezo.

Wabunge wa mataifa ya Tanzania, Burundi, Uganda, Kenya na wenzao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walikuwa na mashindano katika nyanja mbalimbali. Maambukizi sawa na hayo yameripotiwa katika taifa jirani la Uganda ambapo wabunge 50 wamepatikana na virusi hivyo vya Omicron.

Wakati huo huo serikali ya Kenya inasisitiza kuwa watu nchini humo watahitajika kuonesha cheti cha kuchanjwa dhidi ya maambukizi ya Covid-19, ili kupata huduma za serikali, lakini pia kutumia usafiri wa umma.

Katibu katika Wizara ya afya Mercy Mwangangi ametangaza hilo, wakati huu nchi hiyo ikishuhudia ongezeko la maambukizi ambayo kwa sasa yamefikia zaidi ya asilimia 30.

Awali, Mahakama ilikuwa imesitisha agizo hilo la serikali, lililopaswa kuanza kutekelezwa kuanzia Desemba 21, hadi kesi iliyowasilishwa kupinga utartibu huo itakapoamuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.