Pata taarifa kuu
KENYA-CHANJO

Kenya yasiitiza juu ya umuhimu wa chanjo kwa raia wake dhidi ya Covid-19

Serikali ya Kenya inaisisitiza kuwa watu nchini humo watahitajika kuonesha cheti cha kuchanjwa dhidi ya maambukizi ya Covid-19, ili kupata huduma za serikali, lakini pia kutumia usafiri wa umma.

Kenya inaendelea kuripoti visa zaidi vya maambukizi ya virusi vya Corona.
Kenya inaendelea kuripoti visa zaidi vya maambukizi ya virusi vya Corona. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Katibu katika Wizara ya afya Mercy Mwangangi ametangaza hilo, wakati huu nchi hiyo ikishuhudia ongezeko la maambukizi ambayo kwa sasa yamefikia zaidi ya asilimia 30.

Awali, Mahakama ilikuwa imesitisha agizo hilo la serikali, lililopaswa kuanza kutekelezwa kuanzia Desemba 21, hadi kesi iliyowasilishwa kupinga utaratibu huo itakapoamuliwa.

Mahakama ilisitisha mpango uliokuwa umetangazwa na serikali nchini humo kuwazuia watu ambao watakuwa hawajapata chanjo ya kupambana na virusi vya Covid-19 kutopata huduma za serikali na kuingia katika maeneo ya umma kuanzia tarehe 21 mwezi huu.

Mwezi Novemba, serikali kupitia Wizara afya iltangaza kuwa, itakuwa lazima kwa mtu yeyote nchini humo kuonesha cheti kuthibitisha kuwa amepata chanjo, kabla ya kuruhusiwa kupata huduma hospitalini, Shuleni na katika Ofisi za Uhamiaji na utozaji ushuru.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch nalo, lililaani mpango huo wa serikali ya Kenya na kutaka utupiliwe mbali kwa kile lilichosema Kenya haikuwa na chanjo za kutosha kuwachanja watu nchini humo kabla ya muda wa mwisho wa Desemba 21.

Mpaka sasa, Kenya, imewachanja watu wazima Milioni 3.2 ambao wamepata dozi kamili sawa na asilimia 12 ya raia wa nchi hiyo, huku watu wengine zaidi ya Laki 2 na Elfu 50 wakiambukizwa na zaidi Elfu tano Mia tatu wakipoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.