Pata taarifa kuu

Uingereza: Johnson aendelea kusakamwa baada ya kuvunja hatua dhidi ya Covid-19

Nchini Uingereza, imebainika kuwa wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Boris Johnson, walikuwa na sherehe wakati Malkia Elizabeth alipokuwa anamuomboleza mumewe Philip, aliyefarifki dunia mwezi Aprili mwaka uliopita, kitendo ambacho Ofisi hiyo imemwomba radhi Malkia.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Jonhson ashtumiwa kuvunja hatua za kudhibiti Covid-19.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Jonhson ashtumiwa kuvunja hatua za kudhibiti Covid-19. REUTERS/Virginia Mayo/Pool
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari nchini Uingereza, inaongeza shinikizo kwa Boris ambaye anachunguzwa na chama chake kwa kufanya sherehe licha ya mikusanyiko ya watu kuzuiwa kwa sababu ya janga la Covid-19.

Boris amekuwa akipata shinikizo za kujiuzulu kutoka kwa wabunge wa upinzani.

Wiki hii, Boris aliomba radhi bungeni kwa kushiriki kwenye sherehe hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.