Pata taarifa kuu

Corona: Uingereza kupiga marufuku wasafiri kutoka nchi sita za Afrika

Uingereza imetangaza kuwa itapiga marufuku kuingia kwa wasafiri kutoka nchi sita za Afrika, baada ya Afrika Kusini kutangaza ugunduzi wa aina mpya ya Covid-19 yenye mabadiliko mengi. Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe zinahuska na marufuku hiyo.

Wanasayansi wa Uingereza "wanatiwa wasiwasi sana" na aina hii mpya ya Corona, ambayo Afrika Kusini inahusisha ongezeko la hivi karibuni la kesi zilizorekodiwa nchini na ambazo pia zimegunduliwa kwa wasafiri kutoka Botswana au Hong Kong. Walakini, hakuna kesi iliyorekodiwa nchini Uingereza.
Wanasayansi wa Uingereza "wanatiwa wasiwasi sana" na aina hii mpya ya Corona, ambayo Afrika Kusini inahusisha ongezeko la hivi karibuni la kesi zilizorekodiwa nchini na ambazo pia zimegunduliwa kwa wasafiri kutoka Botswana au Hong Kong. Walakini, hakuna kesi iliyorekodiwa nchini Uingereza. © AP/Dmitri Lovetsky
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Afya Sajid Javid amesema safari zote za ndege kutoka Afrika Kusini, Namibia, Lesotho, Eswatini, Zimbabwe na Botswana zitasitishwa kuanzia saa sita usiku leo ijumaa.

"Dalili za kwanza tulizo nazo za aina hii mpya ya Corona ni kwamba inaweza kuambukiza watu zaidi kuliko aina nyingine mpya ya Corona ya Delta na kwamba chanjo tulizo nazo sasa zinaweza kuwa na ufanisi mdogo," amebaini Sajid Javid.

Kulingana na waziri wa afya wa Uingereza, wanasayansi wa Uingereza "wanatiwa wasiwasi sana" na aina hii mpya ya Corona, ambayo Afrika Kusini inahusisha ongezeko la hivi karibuni la kesi zilizorekodiwa nchini na ambazo pia zimegunduliwa kwa wasafiri kutoka Botswana au Hong Kong. Walakini, hakuna kesi iliyorekodiwa nchini Uingereza.

Uingereza ni miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi na Covid-19, baada ya kurekodi vifo 144,000 tangu kuzuka kwa janga hilo. Idadi ya kesi ilikuwa bado iko juu - zaidi ya 47,000 katika kipindi cha saa 24 zilizopita siku ya Alhamisi - lakini zaidi ya 80% ya watu wenye umri wa miaka 12 na zaidi wamepokea sindano mara mbili ya chanjo, na karibu 30% wamepata dozi ya tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.