Pata taarifa kuu

WHO: Ulaya inaweza kukabiliwa na kirusi cha Omicron kama hakuna mikakati bora

Shirika la Afya Duniani, WHO, linaonya kuwa nusu ya watu wanaoishi barani Ulaya, wataambukizwa kirusi kipya cha Covid-19 cha Omicron kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Mkuu wa WHO barani Ulaya Hans Kluge.
Mkuu wa WHO barani Ulaya Hans Kluge. Alberto Pizzoli AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Onyo hili limetolewa na Mkuu wa WHO barani Ulaya Hans Kluge, ambaye amesema idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kwa sababu ya maambukizi makubwa yanayoendelea kushuhudiwa

WHO inasema watu zaidi ya Milioni saba wameambukizwa kirusi aina ya omicron wiki ya kwanza ya mwezi wa Januari.

Wakati huo huo wataalam kutoka Shirika la Afya Duniani wametoa onyo kuhusiana na dozi mpya dhidi ya Covid-19: Kupambana na janga la Covid-19 kwa kutumia dozi za mpay sio mkakati unaofaa, wataalam kutoka Shirika la Afya Duniani wameonya Jumanne hii, Januari 11, pia wakitoa wito wa chanjo ambayo inazuia maambukizi bora.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, kundi hili la wataalam wanaohusika na kusimamia chanjo dhidi ya virusi vya Corona "linabaini kwamba chanjo dhidi ya Covid-19 zina athari kubwa katika suala la uambukizaji na kuzuia maambukizi, pamoja na kuzuia magonjwa na kifo ni lazima na vinapaswa kufanyiwa kazi”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.