Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron: "Wale ambao hawajachanjwa, nataka kukabiliana "

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameonya kuwa watu ambao hawajapata chanjo nchini mwake watapitia kipindi kigumu, katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Covid 19.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Desemba 15, 2021 huko Brussels.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Desemba 15, 2021 huko Brussels. AP - Johanna Geron
Matangazo ya kibiashara

Macron ametoa onyo hilo katika mahojiani na Gazeti la Le Parisien, wakati huu mswada wa sheria, utakaowataka watu kuonesha cheti cha kuchanjwa kuanzia Januari 15 ili kwenda katika maeneo yenye watu wengi kama mikahawani.

Hata hivyo, mswada huo umecheleweshwa kupitishwa na wabunge wa upinzani. Nchini Ufaransa kwa sasa, kirusi cha Omicron kinaendelea kusambaa kwa kasi.

"Mimi, mimi siko hapa kwa ajili ya kuwakasirisha Wafaransa. Ninakabiliana na utawala siku nzima wakati unawazuia kwa jambo fulani. Kweli, wale ambao hawajachanjwa, nataka kukabilian nao. Kwa hivyo tutaendelea kuhamasisha raia kuweza kuchanjwa, hadi mwisho, huo ndio mkakati. "

Emmanuel Macron anakusudia kuweka kikomo "kwao, kwa shughuli za maisha ya kijamii".

Alipoulizwa na msomaji wa gazeti hilo, ambaye alisema kwamba wale ambao hawajachanjwa "ni 85% wanaolazwa katika hospitali", rais wa Ufaransa amebaini kuwa kauli hiyo ndio "hoja bora" kwa mkakati wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.