Pata taarifa kuu

Covid: Nchi mbalimbali Ulaya zarekodi ongezeko kubwa la maambukizi

Mataifa mbalimbali barani Ulaya, yameripoti ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya Covid 19, wakati huu kirusi aina ya Omicron kinapoendelea kusambaa kwa kasi katika bara hilo.

Kufuatia ongezeko la maambukizi haya nchini Ufaransa serikali nchini humo, imetangaza kuwa kuanzia  Januari 3, watu watalazimika kufanyia kazi nyumbani.
Kufuatia ongezeko la maambukizi haya nchini Ufaransa serikali nchini humo, imetangaza kuwa kuanzia Januari 3, watu watalazimika kufanyia kazi nyumbani. AP - Laurent Cipriani
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa imekuwa nchi iliyoripoti maambukizi mapya ya virusi hivyo, baada ya watu karibu 180,000 kupatikana na virusi hivyo siku ya Jumanne pekee.

Hii ndio idadi kubwa ya maambukizi kuwahi kuripotiwa kwa siku moja nchini humo, tangu kuanza kwa janga hilo miaka miwili iliyopita, baada ya kuripoti visa vingine zaidi ya Laki Moja na Elfu nne, Jumamosi iliyopita.

Kufuatia ongezeko la maambukizi haya nchini Ufaransa serikali nchini humo, imetangaza kuwa kuanzia  Januari 3, watu watalazimika kufanyia kazi nyumbani, idadi ya mikusanyiko ya watu kupunguzwa,na watu watahitajika kuthibitisha wamechoma chanjo ili kupatiwa huduma.

Nchini Uingereza, watu karibu  Laki Moja na Elfu thelathini, wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo siku ya Jumanne, huku mataifa mengine kama Ureno, Italia na Ugiriki yakishuhudia ongezeko la maambukizi.

Licha ya kirusi hiki kusambaa kwa kasi, utafiti wa wanasayansi unaonesha kuwa kirusi cha Omicron hakina makali kama kile cha Delta na kati ya asilimia 30 hadi 70 ya watu walioambukizwa ndio hulazwa hospitalini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.