Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAAMBUKIZI

Covid-19: Ufaransa yafikia rekodi ya idadi ya maambukizi

Zaidi ya kesi 94,000 zimerekodia katika kipindi cha saa 24 nchini Ufaransa, idadi ambayo nchi hiyo haijawahi kurekodi kwa kipindi cha siku nzima.

Kituo cha sampuli kwa vipimo vya Covid-19, Ijumaa, Desemba 17, 2021, huko Paris.
Kituo cha sampuli kwa vipimo vya Covid-19, Ijumaa, Desemba 17, 2021, huko Paris. © AP - Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

Kadiri kirusi kipya cha Omicron kinavyoenea, shinikizo kwenye hospitali huongezeka zaidi. Baraza la Ulinzi litakutana Jumatatu kuamua juu ya hatua za kukomesha mlipuko huu wa 5 ambao unaonekana kutodhibitiwa.

Ikiwa na kesi 94,124 za maambukizi katika kipindi cha saa 24, Ufaransa imevuka kwa kiasi kikubwa idadi yake ya juu zaidi ya maambukizi tangu kuzuka kwa janga hilo mwezi Machi 2020.

Mlipuko wa tano unaongezeka na sasa unaonekana kuimarishwa na kirusi kipya kinachoambukiza zaidi cha Omicron. Katika siku saba zilizopita, wastani kulirekodiwa kesi mpya 66,417 kila siku. Takwimu hizi ni dhahiri zina madhara kwa mfumo wa hospitali na ongezeko la waliolazwa katika huduma muhimu, ambayo inapokea wagonjwa 3,254. Kwa jumla, zaidi ya watu 16,000 wamelazwa hospitalini kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.