Pata taarifa kuu

Ufaranza yazidisha vikwazo zaidi dhidi ya Covid

Ufaransa imezidisha hatua kali dhidi ya Covid wakati nchi hiyo ikirekodi zaidi ya maambukizi mapya 100,000 siku ya Jumamosi - idadi kubwa zaidi iliyoripotiwa nchini tangu janga hilo kuzuka.

Jean Castex na Olivier Véran, Jumatatu hii, Desemba 27, 2021 kutoka Matignon.
Jean Castex na Olivier Véran, Jumatatu hii, Desemba 27, 2021 kutoka Matignon. AFP - STEPHANE DE SAKUTIN
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali hiyo Waziri Mkuu Jean Castex ametangaza vikwazo vikali vya Covid huku kukiwa na wasiwasi juu ya kirusi kipya cha Omicron.

Waziri Mkuu wa Ufaransa alielezea hasa Jumatatu hii, Desemba 27 kwamba muda wa chini kabla ya usimamizi wa kipimo cha chanjo dhidi ya Covid-19 utapunguzwa kutoka miezi minne hadi mitatu kuanzia Jumanne hii, kulingana na agizo kutoka kwa Mamlaka ya Afya ya Juu (HAS) lililotolewa Ijumaa, na lenye lengo la kuzuia usambazaji wa kirusi cha Omicron.

Wafaransa wataweza kupokea dozi ya pili au ya tatu ya chanjo dhidi ya Covid kutoka miezi mitatu baada ya chanjo yao ya mwisho na sio miezi minne tena.

"Itatosha kwa miezi mitatu baada ya sindano yako ya pili au ya kwanza ikiwa umekuwa na Covid kunufaika na nyongeza yako", alisema Waziri Mkuu wa Ufaransa Jumatatu wiki hii.

Jean Castex alizungumza kutoka Matignon, Waziri wake wa Afya Olivier Véran akiwa karibu yake, baada ya kufanyika kwa Baraza la Ulinzi la Afya lililoongozwa na Rias, Emmanuel Macron jana Jumatatu.

Idadi ya mikusanyiko kwa watu yapunguzwa

Sheria mpya pia ni pamoja na mipaka ya mikusanyiko ya nje ya umma - ambayo itazuiliwa kwa watu 5,000 - na marufuku ya kula na kunywa kwenye safari za mwendo mrefu.

Vilabu vya usiku vitasalia kufungwa na mikahawa na baa zitaweza kutoa huduma ya mezani pekee. Wafanyikazi wanaofanya kazi nyumbani watalazimika kufanya hivyo angalau siku tatu kwa wiki. Uvaaji wa barakoa utakuwa wa lazima katikati mwa jiji.

Kati ya Wafaransa milioni 45 wanaohusika, karibu nusu tayari wamepokea chanjo. Lengo linabaki kupanua wigo wa chanjo, ili kuzuia aina mbaya za Covid-19 zinazowezekana.

Sheria ya kutotoka nje yatangazwa katika baadhi ya maeneo

Waziri Mkuu hajatangaza sheria ya kutotoka nje kwa jiji kuu, lakini kwa kisiwa cha Reunion, sheria hiyo imetangazwa. Na muda wa sheria ya kutotoka nje huko Martinique pia umeongezwa.

Hata hivyo hakuna kuahirishwa kwa kuanza kwa mwaka wa shule: bado mwaka wa shule umepangwa kuanza Januari 3. Miongoni mwa hatua zingine mpya zilizotangazwa pia ni jukumu la kuvaa barakoa nje ya katikati mwa jiji, lakini pia upanuzi wa muda wa kufanyia kazi nyumbani, hatua ambayo itakuwa ya lazima pale inapowezekana, siku tatu kwa wiki.

Ni lazima kufanyia kazi nyumbani

Kufanyia kazi numbani itakuwa ni la lazima, bila shaka itakuwa ni lazima, katika makampuni yote na kwa wafanyakazi wote ambao inawezekana, angalau siku tatu kwa wiki, na ikiwezekana, siku nne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.