Pata taarifa kuu

Ufaransa kuchukuwa hatua mpya kukabiliana na kirusi cha Omicron

Ufaransa ilivuka rekodi mpya wikendi hii kwa watu walioathiriwa na Covid-19: Zaidi ya visa 100,000 vya maambukizi vilirekodia. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akutana katika kikao cha Baraza la Ulinzi kwa njia ya video na kisha Baraza la Mawaziri Jumatatu alasiri kupitisha hatua mpya kabla ya sikukuu ya Mwaka Mpya.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, katikati, na Waziri wa Afya wa Ufaransa Olivier Véran, kulia, katika hospitali ya La Timone, Alhamisi, Septemba 2, 2021 huko Marseille.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, katikati, na Waziri wa Afya wa Ufaransa Olivier Véran, kulia, katika hospitali ya La Timone, Alhamisi, Septemba 2, 2021 huko Marseille. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Kudhibiti kirusi kipya cha Omicron si chaguo tena. Hata hivyo ni muhimu kupunguza kasi ya maendeleo yake ili kuepuka idadi kubwa ya wagonjwa katika hospitali ambazo zinakabiliwa na idadi kubwa ya wagonjwa walioambukizwa kirusi cha Delta.

Ili kufanya hivyo, serikali inategemea zaidi chanjo: rasimu ya sheria ya kupitisha chanjo inaweza kupitishwa Jumatatu kabla ya kuanza kutumika kabla ya Januari 15. Kuanzia tarehe hiyo, chanjo itakuwa ya lazima kwa kwenda kwenye sinema au kwenye mgahawa.

Masuali mawili kwa hivyo yatajadiliwa wakati wa Baraza la Ulinzi la Afya Jumatatu. Suala la kwanza linahusu muda wa kutotoka nje usiku wa usiku wa Mwaka Mpya pamoja na hatua nyingi ambazo tayari zimeamuliwa kwa jioni hiyo ya mwisho ya mwaka: hakuna fataki zitakazo pigwa, hakuna uuzaji wa pombe na chakula kando ya barabara, ili kuepuka matukio makubwa na bila shaka kufungwa kwa vilabu vya usiku.

Swali la pili litakaloulizwa Jumatatu linahusu wa watu waliotangamana na mgonjwa kuwekwa karantini. Sheria zinazotumika sasa lazima zibadilike, ili kuepusha hali yoyote ya kuzorota kwa shughuli nchini mwanzoni mwa mwezi Januari. Leo, mtu anayeishi na mgonjwa aliyeambukizwa kirusi kipya cha Omicron lazima ajiweke karantini kwa hadi siku 17, hata kama atakuwa hakupatikana na virusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.