Pata taarifa kuu
UINGERZA-EU-MAZUNGUMZO

Mazungumzo ya mwisho kabla ya mkutano muhimu kwa ajili ya EU

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron anaingia Jumatano hii katika mkesha wa mkutano muhimu mjini Brussels, katika mazungumzo ya mwisho ili kuzuia nchi yake isiondoke katika Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker mjini Brussels, Februari 16, 2016.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker mjini Brussels, Februari 16, 2016. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker alikataa kukukbali uwezekano wa kushindwa kwa majadiliano katika kundi la nchi 28.

"Hatuna mpango mwengine, tuna mpango mmoja pekee. Uingereza itabaki katika Umoja wa Ulaya na itakuwa mwanachama muhumu na wa kudumu katika muhumili wa ujenzi wa Umoja wa Ulaya", amesema Bw Juncker, ambaye alimpokea Cameron Jumanne hii katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.

"Kama nilingelisema kwamba tuna mpango mwengine, hali hiyo ingelitoa hisia kwamba inabidi kuwepo na nia ya Tume kufikiria kwamba Uingereza inaweza kuondoka katika Umoja wa Ulaya. Kwa maana hiyo, mimi siingii katika maelezo ya mpango mwengine", amesema Rais wa Tume ya Ulaya, ambaye anajihusisha na kazi kama ya "mpatanishi" katika mazungumzo hayo.

Bw Cameron ameahidi kura ya maoni juu ya kubaki au la kwa nchi yake katika Umoja wa Ulaya. Ana matumaini ya kupata maelewano katika mkutano wa kilele wa marais na viongozi kutoka nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels Alhamisi na Ijumaa wiki hii. Jambo ambalo huenda likapelekea kuandaliwa kwa mashauriano haya katika mwezi wa Juni.

David Cameron pia alikutana na Spika wa Bunge la Ulaya Martin Schulz.

Downing Street amesema katika taarifa kwamba kunasalia "baadhi ya maelezo kuwekwa sawa" baada ya majadiliano kati ya Bw Cameron na viongozi wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.