Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU

Kubaki kwa Uingereza katika EU: Cameron atoa masharti yake

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron atato rasmi Jumanne hii orodha yake ya masharti ya kuibakiza Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Msimamo wake tayari umekwishaoneka.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa Baraza la umoja wa Ulaya Donald Tusk Septemba 24, 2015 jijini Brussels.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa Baraza la umoja wa Ulaya Donald Tusk Septemba 24, 2015 jijini Brussels. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ikidaiwa kwa kinagaubaga na washirika wake kutoa "orodha hiyo" Uingereza hatimaye inatazamia kujibu yaliopendekezwa na Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, ili majibu hayo yaweze kujadiliwa na nchi 28 wanachama wa Baraza la Umoja wa Ulaya mwezi Desemba mjini Brussels. Viongozi hao wawili tayari kuzungumza kwenye simu siku ya Jumatatu ili kujiandalia kikao hicho.

Ili kuishindikiza barua hiyo, David Cameron pia amepanga kuhotubia wananchi wake leo Jumanne asubuhi jijini London, Waziri wake Fedha George Osborne, atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Tume ya Ulaya katika mji mkuu wa Ubelgiji.

Mbio hizo za viongozi hao wawili zimeanzisha utaratibu mwengine wa kutaka ipigwe kura ya maoni juu ya uanachama wa Uingerezakatika Umoja wa Ulaya itafanyika mwishoni mwa mwaka 2017, au mwezi wa Juni 2016.

Tafiti zinaonyesha kugawanyika kwa wanaounga mkono na kupinga uingereza kuendelea kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, wakati ambapo pande zote mbili zimeimarisha kampeni zao tangu mwezi Septemba.

David Cameron, ambaye amesema "hana imani na Umoja wa Ulaya", ametaka kwa upande wake, Uingereza kubaki katika muungano uliyorekebishwa. Lakini kama hakupata mabadiliko anayoyataka, hatobadilisha "lolote" kama alivyoeleza Jumatatu mbele ya washirika wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.