Pata taarifa kuu
UINGEREZA-ELIZABETH II-UTAWALA-SAISA

Elisabeth II avunja rekodi ya miaka mingi katika enzi

Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza ameweka Historia Jumatano wiki hii kwa kuwa katika wadhifa huo kwa muda mrefu.

Elizabeth II, Malkia wa Uingereza, hapa katika mji wa Plymouth, mwezi Machi mwaka 2015.
Elizabeth II, Malkia wa Uingereza, hapa katika mji wa Plymouth, mwezi Machi mwaka 2015. REUTERS/Matt Cardy/Pool
Matangazo ya kibiashara

Malkia Elizabeth wa pili mwenye umri wa miaka 89 alishangiliwa na mamia ya watu alipokuwa anapita katika barabara za jijini la London.

Kufikia leo, Malkia Elizabeth wa pili ametimiza miaka 63 na miezi saba sasa katika enzi, na kuweka historia.

Waziri Mkuu David Cameron ameelezea uongozi wa Malkia Elizabeth wa unyennyekevu mno kwa kipindi chote alichohudumu.

Kabla siku ya Jumatano wiki hii, rekodi ya kuongoza kwa kipindi cha muda mrefu Ufalme wa Uingereza ulikuwa unashikiliwa na Bibi yake Mkuu, Victoria.

Malkia ametumia siku hii pia kufungua rasmi kituo kipya cha reli katika mpaka wa Uingereza na Scotland.

Itafahamika kwamba Elizabeth alitawazwa kuwa malkia akiwa na umri wa miaka 25 pekee.

Mara ya kwanza alipofahamishwa kuwa ndiye atakayekuwa malkia wa Uingereza alikuwa nchini Kenya. Wakati huo alikuwa katika ziara rasmi akiwa na mmewe Philip wakati huo akiwa na umri wa miaka 25 pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.