Pata taarifa kuu
UFARANSA-UINGEREZA-SYRIA-MASHAMBULIZI-USALAMA

Syria: London na Paris waandaa mashambulizi ya anga dhidi ya IS

Kutokana na hatari ya mashambulizi yanayoongozwa kutoka Syria, Ufaransa na Uingereza wamepania kuendesha mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la Islamic State (IS) nchini humo, ambapo London imefanya shambulizi la kwanza ikitumia ndege isio na rubani mwishoni mwa mwezi Agosti.

Rais François Hollande na Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron katika mkutano wa G7 Juni 7, 2015 katika mji wa Garmisch-Partenkirchen.
Rais François Hollande na Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron katika mkutano wa G7 Juni 7, 2015 katika mji wa Garmisch-Partenkirchen. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa itafanya tangu Jumanne wiki hii upelelezi juu ya anga ya Syria," amesema Rais François Hollande Jumatatu wiki hii katika mkutano wake mkuu wa sita na waandishi wa habari. "Upelelezi huo utapelekea kuendesha mashambulizi dhidi ya Daech, kwa kuhifadhi uhuru wetu wa utekelezaji na uamuzi ", amesema rais wa Ufaransa.

" Leo hii nchini Syria, tunachotaka, ni kujua, kufahamu kinachoandaliwa dhidi yetu na kile kinachofanywa dhidi ya watu wa Syria ", ameeleza Rais Hollande, wakati ambapo Ulaya inayokabiliwa na ongezeko kubwa la wahamiaji kutoka Syria, inmeendelea kukumbwa na mgogoro wake mbaya wa uhamiaji tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia.

Kwa upnde wa Ufaransa, lengo ni kupunguza tishio la mashambulizi katika ardhi yake. Mashambulizi yaliosababisha vifo dhidi gazeti la kila wiki la Charlie Hebdo, shambulizi lililofanywa mwishoni mwa mwezi Agosti katika treni ya mwendo wa kasi iliyokua ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Paris (Thalys), shambulizi ambalo lilitibuka, yote hayo yana uhusiano na itikadi kali za kidini na kundi la Islamic State lilikiri kutekeleza baadhi ya mashambulizi.

Upelelezi huo juu ya anga ya Syria utaruhusu Ufaransa kukusanya taarifa ambazo ilishindwa kupata kuhusu vituo vya mafunzo na uamuzi wa kundi la Islamic State nchini Syria.

London Jumatatu ilitoa sababu ya usalama, ikieleza kuwa iliweza kutekeleza shambulizi la anga nchini Syria Agost 21, shambulizi ambalo lililenga ngome za kundi la Islamic State.

“ Wanajihadi watatu, ikiwa ni pamoja na Waingereza wawili, waliuawa katika shambulizi lililoendesha kwa umakini na ndege isio na rubani ya RAF ", Waziri mkuu David Cameron amewaambia wabunge.

" Ilibidi tufanye hivyo kwa sababu watu hao walikuwa wakiajiri na kuandaa mashambulizi ya kijinga dhidi ya nchi za Magharibi. Na kwa sababu katika ukanda huo, hakuna serikali ambayo tunaweza kufanya ushirikiano ", amesema David Cameron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.