Pata taarifa kuu
UFARANSA-SHAMBULIO-IS

Ufaransa: shambulio katika mji wa Isère

Mtu moja ameingia katika kiwanda cha Air Products kinacho milikiwa na na kampuni ya Marekani karibu na mji wa Lyon nchini Ufaransa na kulipua mitungi ya gesi akitumia gari lake. Shambulio hilo limetokea leo Ijumaa saa nne asubuhi.

Mwendesha mashitaka ya mMahakama dhidi ya ugaidi  ameanzisha uchungui kuhusu mashambulizi ya kigaidi kwenye eneo la Air products katika mji wa Saint-Quentin-Fallavier,  Isère, Ijumaa hii, Juni 26 mwaka 2015.
Mwendesha mashitaka ya mMahakama dhidi ya ugaidi ameanzisha uchungui kuhusu mashambulizi ya kigaidi kwenye eneo la Air products katika mji wa Saint-Quentin-Fallavier, Isère, Ijumaa hii, Juni 26 mwaka 2015. Le parquet antiterroriste s'est saisi de l'enquête sur l'attaque
Matangazo ya kibiashara

Mwili wa mtu aliye katwa kichwa umepatikana kwenye mlango wa kuingilia katika kiwanda hicho. Marehemu huyo amejulikana, ni mkuu wa kiwanda cha uchukuzi cha kitongoji kimoja cha Lyon.

Mshukiwa wa mauaji hayo anaitwa Yassin Sahli, Muislamu wa madhehebu ya Salafi, mwenye umri wa zaidi ya miaka thelathini. Amekamatwa baada ya tukio hilo alipokua akijaribu kukimbia. Mke wa mshukiwa huyo na mtu mwengine anayetuhumiwa kuhusika katika mauaji hayo pia wamewekwa chini ya ulinzi. Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve amewasili eneo la tukio.

  • Shambulio limelenga kiwanda kinachomilikiwa na kampuni ya Air Product, ambayo inaundwa na raia wa Marekani. Kampuni hiyo imekua ikitoa gezi na vifaa vya kemikali kwa ajili ya matumizi ya viwanda, katika mji wa Saint-Quentin-Fallavier, karibu na Lyon. Shambulio hilo limetokea muda mfupi kabla ya 10 asubuhi, saa za Ufaransa.
  • Mtu mmoja ameuawa, kwa kukatwa, na kichwa chake kuwekwa juu ya mlango nje ya kiwanda cha Saint-Quentin-Fallavier. Bendera ya wanamgambo wa kiislamuimekua ikizunguka mwli wa mtu huyo. Mtu aliye uawa ni mkuu wa kampuni ya uchukuzi katika kitongoji cha Lyon ambaye aliruhusiwa kuingia katika kampuni ya Ari Product, ambapo mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi na mauaji hayo amekua akiendesha kazi yake.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.